Pata taarifa kuu
MADAGASCAR-HAKI

Madagascar: Wafaransa 2 wahukumiwa kwa jaribio la mapinduzi, Paris yasalia kimya

Mmamlaka nchini Ufaransa inaendelea kusalia kimya baada ya raia wake wawili kuhukumiwa kwa jaribio la mapinduzi nchini Madagascar siku ya Ijumaa.

Katika kesi ya Apollo 21, Jumanne, Desemba 7. Vikosi vya usalama vikishika ulinzi mbele na ndani ya mahakama.
Katika kesi ya Apollo 21, Jumanne, Desemba 7. Vikosi vya usalama vikishika ulinzi mbele na ndani ya mahakama. © S. Tétaud/RFI
Matangazo ya kibiashara

Paul Rafanoharana na Philippe François, afisa wa zamani katika jeshi la Ufaransa, walihukumiwa na mahakama ya Madagascar kwa jaribio la mapinduzi dhidi ya Rais Rajoelina.

Kulingana na mtafiti Olivier Vallée, akihojiwa na Claire Fages, kutoka kitengo cha RFI katika kanda ya Afrika, Paris haitaki kuendelea kuvuruga uhusiano na Antananarivo ambao tayari umedorora.

Nadhani ni ukimya ulioamriwa kwa tahadhari kwa sababu hapo awali, kulikuwa na habari nyingi juu ya ushiriki wa mshauri wa kwanza wa Ufaransa, ambaye ni mtu anayeonekana sana. Kwa upande wa Ufaransa, ilihitajika kwamba kusiwe na upanuzi wa majukumu mengine katika muktadha wa uhusiano na Ikulu ya Madagascar ambao tayari umeorora. Onyo hilo, hasa kwa kumfikisha Victor Ramahatra [Waziri Mkuu wa zamani] mahakamani, liliafikiwa na jeshi la Madagascar. Ni wakati ambao ulifanya iwezekane kusuluhisha tahadhari kadhaa au vitisho kwa serikali iliyopo ambayo sasa inapaswa kuwa na mtazamo wa kuchukuwa dhidi ya wafungwa hao wawili.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.