Pata taarifa kuu
ETHIOPIA-USALAMA

Jeshi la Ethiopia lachukua tena udhibiti wa mji wa Lalibela

Vikosi vya jeshi la Ethiopia vimeudhibiti tena mji wa kihistoria wa Lalibela, siku chache baada ya kutumbukia mikononi mwa waasi wa TPLF. Haijabainika ikiwa kulikuwa na mapigano kati ya waasi na jeshi la serikali kabla ya mji huo kuangoka mikononi mwa vikosi vya jeshi la shirikisho.

Ramani ya Ethiopia ikionyesha eneo la Urithi wa Dunia La Lalibela.
Ramani ya Ethiopia ikionyesha eneo la Urithi wa Dunia La Lalibela. Aude GENET AFP
Matangazo ya kibiashara

Haijafahamika ni lini vikosi vya serikali vilichukua udhibiti wa mji wa Lalibela, lakini mashahidi wanasema wanajeshi wa serikali ndio wanaonekana katika mji huo.

Wakati huo Rais wa jimbo la Tigray, Debretsion Gebremichael amezilaumu Uturuki, Iran na Falme za Kiarabu kwa kuuchochea mgogoro wa nchi hiyo kwa kutoa msaada wa kijeshi na kifedha kwa serikali ya Ethiopia.

Hivi karibuni wakaazi wa mji wa Lalibela waliripoti kwamba wapiganaji wa Tigray walichukua tena udhibiti wa mji huo baada ya jeshi na washirika wake kujiondoa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.