Pata taarifa kuu

Wakimbizi wa Afrika ya Kati warejeshwa makwao kutoka DRC

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR limeanza tena shughuli zake za kuwarejesha makwao wakimbizi kutoka DRC hadi Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Kwenye uwanja wa ndege wa Gbadolite.
Kwenye uwanja wa ndege wa Gbadolite. MONUSCO/Abel Kavanagh
Matangazo ya kibiashara

Jumatatu, Novemba 15, karibu watu 40 waliondoka kwenye kambi ya Inké, karibu na mji wa Gbadolite (Ubangi Kaskazini), kwa ndege ya shirika la kutoa misaada ya kibinadamu kurejea nchini mwao. Kulingana na Umoja wa Mataifa, zaidi ya raia 200,000 wa Jamhuri ya Afrika ya Kati kwa sasa wanaishi katika ardhi ya DRC.

Takriban watu 40 kati yao walikuwa wakisubiri ndege kwenye uwanja wa ndege ... Wanaume, wanawake na watoto waliozaliwa katika jimbo la Nord-Ubangi wamerejeshwa nchini mwao.

Wakimbizi wengi bado wanasita kurudi

Kwa upande wa Giscard, mwenye umri wa miaka 56 kutoka Afrika ya Kati, amesema kurudi kwake nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati "ni siku kuu". "Maisha ya ukimbizini sio mazuri kuliko nyumbani," amesema kwa sauti, akipanda ndege.

Wengi wa raia hao kutoka Jamhuri ya Afrka ya Kati bado wanasita kurejea. Ni chaguo gumu, anaeleza Liz Ahua, mkuu wa UNHCR nchini DRC: “Tunachojua ni kwamba wakimbizi wamefanya uchunguzi kuhusu kile kinachoendelea majumbani mwao. Wameamua kurudi kwa sababu huko walikotoka kuna amani. Watu wanaorejea ni kutoka katika maeneo ya Lobaya na Ombala - Mukoko. "

Wanapofika Jamhuri ya Afrika ya Kati, UNHCR inapanga kuwapa chakula cha kutosha kwa miezi michache, Mohamed Touré, mkuu wa UNHCR katika Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.