Pata taarifa kuu
LIBYA-SIASA

Libya: Saif al-Islam Gaddafi kuwania katika uchaguzi wa urais mwezi Desemba

Mtoto wa aliyekuwa dikteta wa Libya Muammar Gaddafi amewasilisha rasmi faili yake ya kuwania kiti cha urais Jumapili hii, Novemba 14 katika uchaguzi wa urais ncini Libya uliopangwa kufanyika Desemba 24.

Saif al-Islam Gaddafi (kushoto) alikuja kuwasilisha faili yake ya kuwania katika uchaguzi wa urais kwa Tume ya Juu ya Uchaguzi ya Libya. Jumapili Novemba 14, 2021.
Saif al-Islam Gaddafi (kushoto) alikuja kuwasilisha faili yake ya kuwania katika uchaguzi wa urais kwa Tume ya Juu ya Uchaguzi ya Libya. Jumapili Novemba 14, 2021. AFP - STRINGER
Matangazo ya kibiashara

Kugombea huku kwa mtoto wa pili wa Muammar Gaddafi si jambo la kushangaza kwani Seif al-Islam alikwishatangaza nia yake. "Upanga wa Uislamu", hiyo ndiyo maana ya jina lake la kwanza, umerejea rasmi kwenye jukwaa la kisiasa la Libya.

Je kama Libya itaungana tena na Gaddafi? Saif al-Islam, 49, mtoto wa pili wa Muammar Gaddafi, amekuwa akitajwa kwa muda mrefu kama mrithi wa kiongozi huyo wa zamani wa Libya. Katika mahojiano na gazeti la New York Times msimu huu wa joto, tayari alielezea matarajio yake ya kisiasa na nia yake ya "kurudisha umoja uliopotea" wa Libya.

Baada ya kuanguka kwa utawala wa baba yake mwaka 2011 Seif al-Islam alijaribu kuitoroka nchi. Lakini alikamatwa na kikosi cha wanamapinduzi ambacho kilimshikilia kama mfungwa hadi mwaka 2017. Huku wakimlinda, kwa vile watekaji wake walikataa kumfikisha katika mahakama ya Libya, ambayo ilimhukumu kifo mwaka 2015, pamoja na mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita, ambayo ilitaka kumshtaki kwa "uhalifu wa kivita" na "uhalifu dhidi ya binadamu. Hatia na hati ya kukamatwa ambayo inaonekana haikuzuia Tume ya Juu ya Uchaguzi ya Libya kuthibitisha kugombea kwake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.