Pata taarifa kuu
DRC- SIASA

Rais wa DRC Felix Tshisekedi amwidhinisha Denis Kadima kuwa mwenyekiti mpya wa CENI

Rais wa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, Félix TSHISEKEDI amemuidhinisha Denis KADIMA kuwa mwenyekiti mpya wa  Tume ya Uchaguzi CENI, licha ya upinzani wa Kanisa Katoliki na lile la kiprotestanti ikiwa ni pamoja na vyama vya upinzani kama muungano wa Lamuka unaoongozwa naye Martin Fayulu, na FCC inayoungwa mkono na rais wa zamani wa nchi hiyo Jospeh Kabila.

Rais wa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo Felix Tshisekedi wakati akilihutubia taifa Ijumaa Oktoba 22 2021.
Rais wa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo Felix Tshisekedi wakati akilihutubia taifa Ijumaa Oktoba 22 2021. © Ikulu ya Kinshasa DRC
Matangazo ya kibiashara

Akilihutubia taifa hilo usiku wa kuamkia jumamosi hii, Rais Tshisekedi amethibitisha kuwa ameunga mkono uteuzi wa wajumbe 12 kati ya 15 wa ofisi ya CENI ambao watajihusisha na maandalizi ya uchaguzi mkuu unaopangwa kufanyika manmo mwaka 2023.

Ameongeza kuwa ana matumaini" kwamba wajumbe watatu wa upinzani watateuliwa haraka ili kukamilisha ofisi hiyo ya CENI, na kwamba atamteua mtu atakayehusika na ufuatiliaji mzuri wa mchakato wa uchaguzi.

Hii ndio fursa ya kumpongeza rais wa bunge la taifa ambaye ametoa fursa kadhaa kwa madhehebu ya kidini wanachama wa jukwaa husika wakutane ili kupata makubaliano baada ya kutoelewana kuhusu uteuzi wa mwenyekiti mpya. Kwa kuzingatia haya yote hapo juu nimeamua kutia saini hati hiyo inayowateua wanachama wapya wa tume ya uchaguzi CENI, ninawaonya sasa kuharakisha mchakato wa uchaguzi ulio huru na wazi katika muda uliopangwa kikatiba

Upinzani nchini DRC umepinga uteuzi wake Denis Kadima kufuartia kile wananchosema ni mshirika wa karibu wa utawala uliopo madarakani nchini humo.

Katika hatua nyingine chama cha ensemble pour la Republique kinachoongozwa naye Moise Katumbi kimesema pamoja na kusikitishwa na hatua hiyo, bado kinatafakari iwapo kitakubali hatua hiyo ama la, wakati muungano wa Lamuka wake Fayulu ukisisitizia kufanya maandamano ya mara kwa mara kupinga kuidhinishwa kwa Bwana Kadima kuwa mkuu wa Ceni.

Hali ya sintofahamu sasa huenda ikaligubika taifa hilo, ambapo wanasiasa wa upinzani pamoja na kanisa kwa pamoja wameona kuwa uchaguzi unaoandaliwa nchini humo mwaka 2023 upo mashakani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.