Pata taarifa kuu
LIBYA-SIASA

Libya: Wafuasi wa Muammar Gaddafi wana uzito gani katika usawa wa kisiasa?

Mnamo Oktoba 20, 2011, Muammar Gaddafi aliuawa na wenzake kadhaa katika mazingira ambayo bado hayajafafanuliwa. Wafuasi wake walilaani, katika taarifa iliyochapishwa Jumanne, Oktoba 19, "uhalifu wa kivita uliofanywa na NATO". 

Muammar Gaddafi huko Tripoli, Septemba 1, 2011.
Muammar Gaddafi huko Tripoli, Septemba 1, 2011. REUTERS/Zohra Bensemra/Files
Matangazo ya kibiashara

Kamati inayohusika na kumbukumbu ya kifo cha kanali Muammar Gaddafi imetoa wito wa kufanyika kwa mikutano ya ishara ya dakika tano katika miji yote ya Libya. Je! Wafuasi wa Gaddafi wana uzito gani leo katika usawa wa kisiasa wa Libya?

Wafuasi wa utawala wa zamani wanaongeza kasi ya kuonekana kwao hadharani wakati tarehe ya uchaguzi wa urais, uliyopangwa kufayika rasmi Desemba 24, inakaribia, wakipeperusha bendera za kijani na picha za Muammar Gaddafi na mtoto wake Saif al-Islam, ambaye amevunja ukimya wake tangu hivi karibuni.

Wafuasi wa Gaddafi pia wanajihusisha kwa hali na mali katika maisha ya kisiasa. Serikali ya mpito inawajumuisha mawaziri kadhaa wa zamani wakati wa utawala wa Kanali Gaddafi na maafisa kadhaa wa zamani wa jeshi la "Mwongozo wa Mapinduzi" wa Libya sasa wanashirikiana na Marshal Khalifa Haftar.

Maoni yanatofautiana, hata hivyo, juu ya uzito halisi wa Gaddafi. Mbunge Ziad Dgheim anabaini kwamba wamegawanyika, hata kama wanawakilisha, kulingana na kauli, zaidi ya 50% ya raia wa Libya. "Idadi hii ni kubwa mno," amesema Abu al-Kassem Kzeit, mjumbe wa Baraza Kuu la kitaifa. Lakini kwake, anaona kuwa ikiwa Saif al-Islam ataruhusiwa kujitwania katika uchaguzi wa urais, ataweza kuunganisha zaidi ya wafuasi wake.

Kwa mujibu wa mtafiti Jalel Harchaoui, nadharia ya Gaddafi ni muhimu, lakini po kwa "njia iliyotawanyika." Wazo la kuwa na "kambi moja ya kijani kibichi, imara na yenye usawa haipo", ameongeza.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.