Ufugaji na uvunaji wa asali kwa njia ya kisasa Wilayani Kabalo nchini DRC
Ufugaji wa nyuki kwa ajili ya kupata asali, kwa ajili ya kiuchumi, umeanza kupata umaarufu katika eneo la Kabalo, mkoani Tanganyika nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Imechapishwa:
Cheza - 01:48
Kihistoria shughuli za ufugaji wa nyuki kwa ajili ya asali, imekuwa ikitekelezwa na makabila ya Twa na Bantu kwa ajili ya matumizi yao kama chakula kikuu na kuuza ili kujipatia kipato.
Hata hivyo, wafungaji hao sasa wana cha kufurahia baada ya Shirika lisilo la kiserikali kutoka nchini Ufaransa, Apiflordev, kuwapa mbinu za kisasa za kufuga nyuki na kuvuna asali.
Medard Sibangolo, Mkuu wa kitengo cha Kilimo katika Wilaya ya Kabalo anaeleza kuhusu mbinu hii mpya.
Tunaangalia katika mziga huu wa kuvuna asali, tunaufungua na kupata asali ndani, sasa tunavuna.
Daniel Mbuyu, mmoja wa mfugaji wa asali kutumia njia ya kisasa anaeleza manufaa ya njia hii mpya.
Njia za zamani zilikuwa zinachosha sana, kwa sababu ulitakiwa kwenda msituni na moshi na moto ili kupata nyuki, lakini kwa sasa tunaweza kufanya hili na kuwaacha nyuki na kuvua vizuri.
Londres Sango, afisa wa mipango kutoka Shirika la Chakula na Kilimo FAO katika eneo hilo, anazungumzia manufaa ya mbinu hii ya kisasa.
Tunavuna asali mara mbili kwa mwaka. Tukipata kiwango kidogo hasa mwezi Aprili, tunapata Lita 15 kutoka kwenye kila mzinga. Lakini katika msimu mkubwa, tunapata Lita 15 hadi 20 na huo ni mwezi wa Oktoba.
Mpaka sasa, mizinga ya kuvuna asali 570 imewekwa kwenye Wilaya ya Kabalo na sasa Shirika la FAO linasema, litafungua soko la asali katika mji huo ili kuimarisha biashara ya biadhaa hiyo.