Pata taarifa kuu
SUDAN-SIASA

Sudan: Wanajeshi na raia washtumiana kwa jaribio la mapinduzi

Nchini Sudan, kumeibuka maswali kuhusiana na mapinduzi yaliyotibuliwa siku ya Jumanne wiki hii. Pande mbili, wanajeshi na raia wamekuwa wanashtumiana kila upande kuhusika katika jaribio hilo.

Jenerali "Hemeti" na Waziri Mkuu Abdallah Hamdok wanashtumiana kwa jaribio la mapinduzi nchini Sudan (Picha ya kumbukumbu).
Jenerali "Hemeti" na Waziri Mkuu Abdallah Hamdok wanashtumiana kwa jaribio la mapinduzi nchini Sudan (Picha ya kumbukumbu). © EBRAHIM HAMID/AFP
Matangazo ya kibiashara

Viongozi wa Sudan wamewahusisha wafuasi wa rais wa zamani wa nchi hiyo Omar al-Bashir katika jaribio hilo, na hivyo kuonyesha wazi udhaifu wa taasisi za mpito. Hali hii inaonyesha mgawanyiko kati ya raia na wanajeshi walio katika taasisi hizi za mpito.

Licha ya nyimbo za kizalendo zilizopigwa kwenye runinga ya taifa Jumanne, mgawanyiko unaoneskana dhahiri katika taasisi za mpito na jaribio hili la mapinduzi lililotibuliwa, limeonyesha ukweli wa jambo hili .

Kuanzia Jumanne, nambari 2 wa Baraza Kuu la Utawala, mkuu wa jeshi Mohamed Hamdan Dagalo, anayejulikana kama "Hemeti" aliwatuhumu "wanasiasa", kwa kuhusika moja kwa moja. Jumatano, alirejelea kauli hiyo, alipokuwa akizuru kambi ya jeshi, akiwatuhumu wanasiasa hawa kuwa "wamepuuzia raia na huduma za msingi", pia "wanajihusisha tu na kupigania madaraka", hali ambayo "ilisababisha kwa jumla raia kupandwa na hasira" na kutoa fursa "kwa jaribio hili lililoshindwa.

Waziri Mkuu Abdallah Hamdok, kiongozi wa kiraia katika serikali hii ya mpito, amepingana na kauli hiyo: anaona mapinduzi haya yaliyotibuliwa yaliyotokana hasa na maafisa wa jeshi, ushahidi ni kwamba ni muhimu kuendeleza mageuzi katika sekta ya usalama.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.