Pata taarifa kuu
DRC-USALAMA

DRC yamshikilia mkufunzi wa waasi wa ADF

Raia wa kigeni kutoka Jordan, aliyeoneshwa na mamlaka ya DRC kama mkufunzi wa waasi wa kundi la waas la Allied Democratic Forces (ADF) anashikiliwa na idara za usalama, baada ya kukamatwa kwenye barabara hatari huko Beni, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, chanzo cha serikali kimebaini, kulingana tovuti ya VOA Afrique.

Eringeti, eneo la Beni, Kivu ya Kaskazini, DR Congo. Desemba 5, 2014: Mwanajeshi wa kikosi cha wanajeshi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (FARDC).
Eringeti, eneo la Beni, Kivu ya Kaskazini, DR Congo. Desemba 5, 2014: Mwanajeshi wa kikosi cha wanajeshi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (FARDC). MONUSCO/Abel Kavanagh
Matangazo ya kibiashara

"Jeshi lilimkamata raia wa Jordan katika barabara ya Beni-Kasindi. Alihamishiwa Kinshasa na alihojiwa leo (Jumanne) na ofisi ya mwendesha mashtaka katika mahakama ya kijeshi," msemaji wa serikali ya DRC Patrick Muyaya ameliambia shirika la habari la AFP, kulingana na VOA Afrique.

"Mtu huyu alikuwa na jukumu la kuwafundisha magaidi wa ADF jinsi ya kutumia ndege zisizo na rubani," ameongeza.

Kulingana na chanzo kingine, alikuwa na kibali cha makazi kutoka Jamhuri ya Kosovo. Hati hii inaonyesha umri wake, miaka 40, na inataja uraia wake (Saudi Arabia) badala ya Jordan kama alivyodai mwenyewe alipokamatwa.

Mnamo Mei, mateka wa zamani wa ADF alishuhudia kwa timu ya shirika la habari la AFP kuwa aliona raia wa kigeni wakifundisha waasi wa ADF jinsi ya kutumia ndege zisizo na rubani kwenye eneo la msitu katika eneo la Beni.

Kati ya mamia ya makundi yenye silaha yaliyo katika eneo la mashariki mwa DRC, ADF wanatuhumiwa kuhusika na mauaji ya raia zaidi ya 6,000 tangu mwaka 2013, kulingana na hesabu kutoka maaskofu wa DRC. Awali, ADF walikuwa waasi wa Kiislamu wa Uganda. Leo inadaiwa kuwa ni tawi la kundi la ISlamic State IS) katika Afrika ya Kati.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.