Pata taarifa kuu
SOMALIA-SIASA

Somalia: Rais Farmajo na Waziri Mkuu wake washindwa kuelewana

Mgogoro kati ya rais wa Somalia Mohamed Abdullah Mohamed Farmajo, na Waziri wake Mkuu Mohammed Hussein Roble unazidi kuongezeka wakati nchi hii inajiandaa kufanya uchaguzi wa urais mwezi Oktoba 2021.

Rais wa Somalia Mohamed Abdullahi Farmajo huko Mogadishu baada tu ya uchaguzi wake,  Februari 8, 2017.
Rais wa Somalia Mohamed Abdullahi Farmajo huko Mogadishu baada tu ya uchaguzi wake, Februari 8, 2017. AP - Farah Abdi Warsameh
Matangazo ya kibiashara

Mgogoro huo ulianza mapema mwaka huu, wakati rais Mohamed Abdullah Mohamed alipoongeza muhula wake kwa miaka miwili, ambao tayari ulikuwa umemalizika, lakini ulizuka baada ya kuuawa kwa afisa wa idara ya ujasusi mnamo mwezi Juni mwaka jana.

Mbele ya ujumbe wa Umoja wa Mataifa, uliozuru Mogadishu Jumapili hii, Septemba 12, Waziri Mkuu alitoa wito tena wa uchunguzi "wa kuaminika" kuhusu tukio hili. Aliomba vizuizi vyote viondolewe ili kupata wahalifu. Shtaka ambalo kwa linamlenga kwa njia moja ama nyingine mkurugenzi wa idara ya ujasusi, lakini pia rais Farmajo, amaye anashukiwa kupinga uchunguzi huu.

Siku kumi zilizopita, Waziri Mkuu alimfuta kazi mkuu wa idara ya ujasusi (Nisa), Fahad Yasin, akibini kwamba hakubaliani na matokeo ya uchunguzi wake juu ya kutoweka kwa Ikran Tahlil Farah, 25. Mtaalam huyu wa usalama wa mtandao katika idara ya ujasusi ya Somalia alitekwa nyara mnamo Juni 26 karibu na nyumba yake huko Mogadishu, kisha kuteswa na kuuawa.

Jumuiya ya kimataifa ina wasiwasi

Kufutwa kazi kwa afisa huyo mwandamizi hakukumfurahisha Mkuu wa Nchi ambaye alibatilisha uamuzi huu "ulio kinyme cha sheria na kinyume cha katiba", kisha akateua mtu mwengine kushikilia nafasi hiyo kama mkuu wa Nisa, baada ya kumpandisha cheo Fahad Yasin kama mshauri wa usalama wa kitaifa. Siku ya Jumatano, mvutano mpya ulizuka wakati Waziri Mkuu alipotangaza kumfuta kazi Waziri wa Usalama, na badala yake kukosolewa na Farmajo.

Maamuzi ambayo kwa hivyo yaliongeza mvutano kati ya wawili hao. Tangu wakati huo, rais na waziri wake mkuu wamekutana mara kadhaa kwakujaribu kusitisha mvutano, lakini bila mafanikio. Jumuiya ya kimataifa ina wasiwasi juu ya mgogoro huu kwani Somalia inatarajiwa kufanya uchaguzi wa urais chini ya mwezi mmoja.

Jumapili hii, mbele ya ujumbe huo wa Umoja wa Mataifa, Waziri Mkuu alihakikisha kwamba uchaguzi wa urais utafanyika kama ilivyopangwa, licha ya mvutano huo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.