Pata taarifa kuu
AFRIKA KUSINI

Covid-19 Afrika Kusini: Chanjo yafunguliwa kwa watu wazima wote

Afrika Kusini imefungua chanjo kwa watu wazima wote wikendi hii. Nchi inaendelea kurekodi karibu visa vipya 13,000 vya maambukizi ya virusi vya Corona kwa siku na 8% tu ya raia wamepewa chanjo kamili.

Afrika Kusini imefungua chanjo kwa watu wazima wote na inatarajia kufikia malengo yake ya 70% ya watu wazima waliopewa chanjo ifikapo mwishoni mwa mwaka huu.
Afrika Kusini imefungua chanjo kwa watu wazima wote na inatarajia kufikia malengo yake ya 70% ya watu wazima waliopewa chanjo ifikapo mwishoni mwa mwaka huu. Luis ROBAYO AFP/File
Matangazo ya kibiashara

Ingawa 72% ya raia wa Afrika Kusini waliofanyiwa utafiti katika Chuo Kikuu cha Johannesburg wanasema wako tayari 'kukubali' chanjo, zoezi la kutoa chanjo katika vituo vya chanjo haliendeshwi vya kutosha kutarajia kufikia lengo lililowekwa la 70% ya watu wazima waliopewa chanjo , ifikapo mwishoni mwa mwaka huu. Serikali inatarajia kuharakisha zoezi hilo kwa kufanya mchakato kupatikana zaidi.

Ili kuwezesha zoezi hilo kwa wotu wote, vituovya chanjo wimeekwa kila mahali mitaani, hata katika vituo vya magari kama vile jijini Soweto. 

"Tuligundua kuwa watu hawaripoti kwenye vituo vya chanjo. Kwa hivyo tumewasogezea karibu yao vituo hivyo. Watu wengi hukusanyika hapa kutoka sehemu nyingi na ni rahisi kwao, kabla ya kuchukua teksi, kusimama na kupata chanjo. Vivyo hivyo kwa madereva. Wanaweza kwenda kupata chanjo kwa urahisi, " amesema Zodwa Malamule anayesimamia shughuli hizo.

"Nimekuja na baba yangu. Ana umri wa miaka 59 na ndiye aliyetuhimiza kwamba tuje kupata chanjo mara moja na kwa sababu tulikuwa tukingojea fursa hiyo. Ni chanjo ya familia, " mesema Ephraim, 32, mmoja wa watu waliopewa chanjo hdidi ya Corona.

Mipango mingine iimewekwa kuwezesha watu kupata chanjo kwa urahisi, kama vile kuweka treni kwenda kuchanja watu katika maeneo ya mbali zaidi nchini.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.