Pata taarifa kuu
ETHIOPIA-USALAMA

Makundi ya waasi wa Oroma na Tigray yajaribu kuungana kuiangusha serikali ya Ethiopia

Serikali ya Ethiopia, imelaani ripoti ya kundi linalosema ni la kigaidi la Oromo Liberation Army kutangaza kuungana na waasi wa jimbo la Tigray, kuendeleza vita nchini humo kwa lengo la kuiangusha serikali ya Waziri Mkuu Abiy Ahmed.

Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed.
Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed. AP - Mulugeta Ayene
Matangazo ya kibiashara

Kiongozi wa jeshi la ukombozi wa Tigray TPLF, Debretsion Gebremichael ameliambia shirika la habari la Reuters kwamba wanafanya mazunguzo na jeshi la waasi wa jimbo la Oromo.

Msemaji wa jeshi la waasi wa Oromo Odaa Tarbii pia amethibitisha kuwa pande mbili hizo zinashirikiana katika mambo ya upelelezi na katika kuratibisha mikakati. Serikali kuu ya Ethiopia haijasema chochote juu ya habari hizo.

Wiki hii, Waziri Mkuu Abiy Ahmed, alitoa wito kwa raia kuungana na jeshi la nchi hiyo kupambana na waasi wa Tigray wanaoendeleza vita nchini humo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.