Pata taarifa kuu
ETHIOPIA

Vita Ethiopia: Abiy Ahmed ataka raia kujiunga na jeshi katika vita dhidi ya TPLF

Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed ametoa wito kwa "Waethiopia wote wenye nguvu na wazima" kujiunga na vikosi vya jeshi, kwani mzozo wa miezi tisa huko Tigray umeenea katika wiki za hivi karibuni kwa mikoa miwili jirani kaskazini mwa nchi.

Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed.
Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed. AP - Mulugeta Ayene
Matangazo ya kibiashara

"Huu ni wakati wa Waethiopia wote wenye umri kamili kuweza kujiunga na vikosi vya ulinzi, vikosi maalum na wanamgambo na kuonyesha uzalendo wao," imesema ofisi ya waziri mkuu, ambaye katika siku za hivi karibuni, alitangaza kusitisha.

Mgogoro huko Tigray umebadili taswira na kuwashangaza wengi tangu mwishoni mwamwezi Juni.

Mapigano hayo yalianza mwezi wa Novemba uliyopita baada ya Waziri Mkuu Abiy Ahmed kupeleka jeshi la shirikisho katika jimbo la Tigray kuwatimua madarakati viongozi wa jimbo hilo, ambao ni kutoka chama cha Tigray People's Liberation Front (TPLF).

Kulingana na mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel ya 2019, operesheni hii ilikuwa kujibu mashambulio kwenye kambi za jeshi la shirikisho zilizovamiwa na waasi wa TPLF. Bwana Abiy alitangaza ushindi mwishoni mwa mwezi Novemba baada ya kutekwa kwa mji mkuu wa mkoa, Mekele.

Lakini Juni 28, vikosi vya waasi wanaounga mkono TPLF waliudhibiti mji wa Mekele, kisha sehemu kubwa ya Tigray kwa siku zilizofuata.

Baada ya usitishaji mapigano uliotangazwa na Abiy Ahmed, kwa sababu rasmi za kibinadamu, na kuondolewa kwa wanajeshi wa Ethiopia, vikosi vya TPLF viliendelea na mashambulio yao kuelekea maeneo jirani ya Amhara, kusini, na Afar, Mashariki.

TPLF imesisitiza kuwa haitaki kuteka eneo la Amhara na Afar, lakini kwamba inataka kuwezesha upatikanaji wa misaada ya kibinadamu katika eneo hilo na kuzuia vikosi vinavyounga mkono serikali kujipanga tena.

Miezi tisa ya mzozo imesababisha vifo vya maelfu ya watu na makumi ya maelfu wkuyatoroka  makazi yao. Hali ya kibinadamu huko ni mbaya.

Karibu watu 400,000 wanaishi katika mazingira ya njaa huko Tigray, kulingana na Umoja wa Mataifa.

Siku ya Jumatatu, WFP ilisema watu 300,000 sasa wanakabiliwa na uhaba wa chakula katika maeneo ya Afar na Amhara.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.