Pata taarifa kuu
SUDAN-ETHIOPIA

Khartoum na Addis Ababa zaendelea kuvutana

Wizara ya Mambo ya Nje ya Sudan, imemwita nyumbani balozi wake nchini Ethiopia kwa mashauriano baada ya Ethiopia kukataa mpango wa Sudan kusuluhisha mapigano kwenye eneo la Tigray.

Waziri mkuu wa Sudan, Abdallah Hamdock
Waziri mkuu wa Sudan, Abdallah Hamdock ASHRAF SHAZLY / AFP
Matangazo ya kibiashara

Katika taarifa, wizara ya Mambo ya Nje ya Sudan imesema, waziri mkuu Abdalla Hamdock, ambaye pia ni mweneyekiti wa IGAD alikuwa na nia ya kuzishawishi pande hasimu nchini Ethiopia kusuluhisha vita vya Tigray. 

Aidha taarifa hiyo imesema nia ya Sudan katika kutatua mzozo wa Tigray ni sehemu ya kujitolea kwake katika kuleta amani na utulivu katika ukanda huo. 

Juma lililopita, Ethiopia ilisema kuwa haina imani na baadhi ya viongozi wa Sudan, huku ikilituhumu jeshi la Sudan kwa kutumia mgogogro wa Tigray kama fursa ya kuingia Ethiopia. 

Uhusiano baina ya utawala wa Khartoum na Addis Ababa umeonekana kudorora kutokana eneo la Fashaga linalozozaniwa na mataifa hayo mawili. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.