Pata taarifa kuu
DRC-TSHISEKEDI-CENI

DRC yaanza mchakato wa kuigeuza Tume ya Uchaguzi CENI

Miaka miwili kabla ya uchaguzi mkuu nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, rais wa nchi hiyo Felix Tshisekedi ametangaza sheria inayoagiza mageuzi ya muundo wa tume huru ya uchaguzi CENI ambapo bila shaka inavyoonekana siasa itabaki kuwa na mkono ndani yake.

Tume ya Uchaguzi nchini DRC CENI
Tume ya Uchaguzi nchini DRC CENI Caroline Thirion / AFP
Matangazo ya kibiashara

Rais Felix Tshisekedi ametangaza sheria inayoziagiza mageuzi ya tume huru ya uchaguzi CENI.

Awali, wanasiasa wa upinzani walieleza wazi kwamba kuchapishwa kwa sheria hiyo juu ya upangaji na utendaji wa Tume Huru ya Kitaifa ya Uchaguzi (CENI), kama ilivyorekebishwa na Bunge na Seneti.

Kutangazwa na rais wa Jamhuri, inaonesha ni kiasi gani siasa itakuwa na mkono kwenye tume hiyo na kuandaa udanganyifu katika uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2023.

Hata hivyo wabunge kutoka muungano wa Union Sacree wamebaini kuwa rais wa Jamhuri amefuata utaratibu uliowekwa ndani ya katiba.

Upande wake Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa UN nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo,  Bintou Keita, wakati akiwasilisha ripoti yake juu ya hali nchini DRC kwa katibu mkuu amesema kuelekea katika uchaguzi wa 2023, ni muhimu  makubaliano ya kitaifa yapatikane juu ya uteuzi wa maafisa wa CENI.

Amesisitiza kuwa uchaguzi uliopangwa kufanyika 2023 upangwe kwa wakati na kwa njia ya makubaliano.

Bintu Keita amewatolea wito wadau wote wa kisiasa na wale walio katika mashirika ya kiraia kuweka juhudi zao kwa pamoja kufaanikisha huru na wa kuaminika.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.