Pata taarifa kuu

DRC: Maswali zaidi kuhusu uhusiano wa ADF na IS

Msikilizaji kwa mujibu wa ripoti mpya za mashirika yanayofuatilia hali ya usalama mashariki mwa nchi ya DRC, yanasema ni wazi kundi la waasi wa ADF lina uhusiano wakaribu na kundi la Islamic State.

Wanajeshi wa nchi ya Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Wanajeshi wa nchi ya Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. © Stringer / Reuters
Matangazo ya kibiashara

Licha ya kuwa hadi sasa wataalamu wa masuala ya usalama hawajaweza kulihusisha moja kwa moja na kundi la Islamic State, lakini wanaamini vitendo vinavyofaywa na waasi hao wa Uganda, vinalingana kabisa na vile vya wanajihadi wa IS.

 

Kwa mujibu wa shirika ma Kivu Security Tracker, kundi la ADF ni miongoni mwa makundi zaidi ya 122 yanayofanya shughuli zao mashariki mwa DRC.

 

Kanisa katoliki nchini humo linasema waasi hao wameua watu zaidi ya elfu 6 tangu mwaka 2013, huku shirika la Kivu Security Tracker, likiwataja waasi hao kuhusika na mauaji ya watu zaidi ya elfu 1 na 200.

 

Juma lililopita mji wa Beni ulishuhudia mashambuli ya mabomu yaliyolenga makanisa na sehemu za burudani.

 

Machi 10 mwaka huu nchi ya Marekani, ililiorodhesha kundi hilo kama mtandao wa kigaidi, unaoongozwa na Seka Musa Baluku.

 

Kundi la IS linahusishwa na uasi kwenye nchi za Sahel na Msumbiji, huku umoja wa Mataifa ukisema bado unafuatilia mwenendo wa kundi hilo kujua ikiwa linauhusiano wa moja kwa moja na IS.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.