Pata taarifa kuu

DRC: Rais wa zamani wa Ivory Coast, Laurent Gbagbo akutana na Rais Tshisekedi, Kinshasa

Rais wa wa zamani wa Ivory Coast, Laurent Gbagbo, mwishoni mwa juma amekutana na Rais wa DRC, Felix Tshisekedi, wakati wa sherehe ya ndoa ya mtoto wa makamu wa rais wa zamani Jean-Pierre Bemba, jijini Kinshasa.

Rais wa zamani wa Ivory Coast, Laurent Gbagbo. Picha hii ni ya maktaba.
Rais wa zamani wa Ivory Coast, Laurent Gbagbo. Picha hii ni ya maktaba. AP - Jerry Lampen
Matangazo ya kibiashara

Bemba, mbabe wa zamani wa kivita na aliyewahi kuwa makamu wa rais, alikutana na Gbagbo, katika jela ya mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita ICC mjini The Hague, ambako wote walishtakiwa kwa tuhuma za makos aya uhalifu wa kivita.

 

Kwa mujibu wa mwandishi wetu wa Kinshasa, Patient Ligodi, rais Tshisekedi alikutana ana kwa ana na Gbagbo, katika sherehe ya mtoto wa Bemba, Jean-Emmanuel bemba ambaye alikuwa akifunga ndoa.

 

Kwa mujibu wa mwanahabari huyo, viongozi hao hawakuzungumza kwa muda mrefu ingawa walisalimiana na kuzungumza machache.

 

Vyanzo vya karibu na rais Tshisekedi, vinasema ni wakatu huu walipokutana, kiongozi wan chi alimualika katika ikulu yake kiongozi huyo wa zamani wa Ivory Coast kwa mazungumzo zaidi.

 

Taarifa zaidi zinasema viongozi hao walikutana kwa mazungumzo ya kina siku ya Jumapili, ambapo pia alimualika Bemba na wake kuhudhuria mazungumzo hayo na kupata chakula cha jioni.

 

Gbagbo, aliwasili nchini DRC siku ya Ijumaa iliyopita kwa mwaliko wa Bemba, ambaye alimuomba kuhudhuria sherehe ya harusi ya mtoto wake.

 

Tangu awasili nchini humo, Rais Gbagbo, alipewa heshima zote kama rais mstaafu kuanzia alipowasili katika uwanja wa ndege wa Kinshasa, ambapo baada ya mapumziko ya siku kadhaa, anatarajiwa kurejea nchini mwake Julai 8.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.