Pata taarifa kuu
ETHIOPIA - SIASA

Ethiopia - Abiy Ahmed atetea hatua ya wanajeshi wake kuondoka Tigray

Waziri mkuu wa Ethiopia, Abiy Ahmed, ametetea uamuzi wa wanajeshi wake kuondoka kwenye mji wa Mekele, jimboni Tigray,  akisisitiza wana uwezo wa kuuchukua mji huo wakati wowote kutoka kwa vikosi vya TPLF ambavyo vimerejea baada ya wanajeshi wa Serikali kuondoka kwenye mji huo.

Waziri mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed
Waziri mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed Facebook page of Abiy Ahmed/AFP
Matangazo ya kibiashara

Abiy Ahmed, amesema vikosi vya eneo hilo havina nguvu tena kama ilivyokuwa wakati wakianza kutekeleza operesheni za kijeshi kwenye eneo la Tigray.

Hata hivyo msemaji wa TPLF, Getachew Reda, amekanusha kauli ya Abiy kwamba wanajeshi wa Ethiopia walijiondoa wakidai kuwa wapiganaji wa TPLF waliwaondoa jimboni Tigray.

Reda anasema, wapiganaji wake wataendelea kupambana na vikosi vya serikali hadi pale watarejesha kabisa udhibiti wa jimbo wa Tigray.

Reda ameongeza kuwa hawatashiriki mazungumzo na serikali ya Ethiopia hadi pale  itaporejesha huduma za mawasiliano, usafiri na huduma nyingine muhimu zilizokatizwa wakati wa mapigano.

Jumanne ya juma hili wapiganaji wa TPLF, walitangaza kuchukuwa tena udhibiti wa mji mkuu wa jimbo la Tigray, Mekelle, wakiapa kuwaondoa wanajesho wote wa Ethiopia na Eritrea ambao wamekuwa katika jimbo hilo kwa miezi nane.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.