Pata taarifa kuu
KENYA - SIASA

Kenya - Mahakama yaanza kusikiliza rufaa ya BBI

Mahakama ya rufaa nchini Kenya, imeanza kuskiza rufaa ya kesi  iliotupwa nje na makama kuu kuhusiana na hatua ya serikali kutaka kufanyia marekebisho katiba ya taifa hilo, kupitia mpango wa kuwaunganisha wakenya wa Building Bridges Initiative, maarufu kama (BBI).

Mahakama ya juu nchini Kenya
Mahakama ya juu nchini Kenya REUTERS/Baz Ratner
Matangazo ya kibiashara

Jopo la majaji watano limeanza leo kuskiza kesi hiyo kwa siku tano, maamuzi ya kesi hiyo yakitarajiwa kubaini iwapo Kenya, itashiriki kura ya maoni kubadilisha katiba au la.

Jopo hilo la majaji linaongozwa na rais wa mahakama ya rufaa, jaji Daniel Musinga, jaji Roselyn nambuye, Hannah Okwengu, Patrick Kiage, Gatembu Kairu, Fatuma Sichale na Francis Tuiyott.

Wazilishi wa marekebisho hayo ya katiba wakiongozwa na rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta na Kiongozi wa Upinzani, Raila Odinga, wanaitaka mahakama ya rufaa kufuta uamuzi wa mahakama kuu na kuruhusu kura ya maoni kufanyika, ili katiba ya Kenya ifanyiwe marekebisho, ambapo rais atakuwa na uwezo wa kumteuwa waziri mkuu na maafisa wengine wa serikali miongoni mwa marekebisho mengine.

Rais Kenyatta, na Odinga, wanasema njia pekee ya kuzia Kenya kushuhudia machafuko ya kila baada ya uchaguzi, ni kubadilisha katiba ya taifa hilo.

Mahakama kuu ilizuia kura ya maoni kufanyika kutoka na sababu kadhaa ikiwemo kutofuata sheria wakati wa kuanzishwa kwa mchakato mzima wa kufanyia katiba marekebisho.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.