Pata taarifa kuu
CAR-UMOJA WA MATAIFA

Umoja wa mataifa UN wakosoa uwepo wa mamluki wa Urusi nchini Jamhuri ya Afrika ya kati

Nchi zenye kura ya veto katika Baraza la usalama la umoja wa mataifa kama Marekani, Uingereza na Ufaransa Jumatano, ya Juni 23, ziliwatuhumu mamluki wa Urusi kwa kuendeleza vitendo vya ukiukaji wa haki za binadamu wakati wakishirikiana na vikosi vya serikali ya Jamhuri ya Afrika ya Kati, hali ambayo imezua mvutano kati ya tume ya umoja wa mataifa Minuscana serikali ya Bangui.

Helikopta ya vikosi vya Urusi na gari la tume ya umoja wa mataifa UN katika nchi ya Jamhuri ya Afrika ya Kati mnamo Januari 10, 2021.
Helikopta ya vikosi vya Urusi na gari la tume ya umoja wa mataifa UN katika nchi ya Jamhuri ya Afrika ya Kati mnamo Januari 10, 2021. © RFI - Charlotte Cosset
Matangazo ya kibiashara

Akizungumza wakati wa mkutano wa wajumbe wa baraza la usalama la umoja wa mataifa, mjumbe maalumu wa umoja huo kwa ajili ya Jamhuri ya Afrika ya Kati, Mankeur Ndiaye, amefahamisha kuwa kumekuwa na wasiwasi mkubwa kuhusu shughuli za kijeshi zinazofanywa na jeshi la taifa hilo pamoja na vikosi washirika kama vile vya Urusi katika mapambano dhidi ya makundi ya waasi yanayomuunga mkono rais wa zamani wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, Francois Bozize.

Ndiaye amesema hali inayoshuhudia hivi sasa nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati ni ya kusikitisha sana na kwamba jeshi la nchi hiyo pamoja na washirika wao wamekuwa wakijihusisha na vitendo vya ukiukaji wa haki za binadamu, kuvunjwa kwa sheria za kimataifa na kwamba kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa nchini humo MINUSCA hakishirikishwi tena kama hapo awali.

Baraza la usalama la umoja wa mataifa linasema kumekuwa utumiaji wa nguvu kupita kiasi upande wa wanajeshi wa serikali na washirika wao, katika operesheni nyingi zinazolenga kuwatokomeza waasi

Mkuu wa Minusca ameitaka umoja wa mataifa kuchukua hatua mapema dhidi ya Jamhuri ya Afrika ya kati kabla ya kuharibika kwa hali ya kibinadamu nchini humo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.