Pata taarifa kuu

Kamati inayohusika na kuteua wanachama wa Baraza la Mpito la Kitaifa yaundwa nchini Tchad

Kamati inayohusika na uteuzi wa wanachama wa siku za usoni wa Baraza la Mpito la Kitaifa (CNT) iimeundwa kwa amri Juni 13, 2021. CNT itatumika kama Bunge kwa miezi 16 iliyobaki ya mpito. Wajumbe haswa watahusika na kuandaa Katiba mpya.

Jenerali Djimadoum Tiraina, makamu wa rais wa Baraza la Jeshi la Mpito, huko Ndjamena, Aprili 21, 2021.
Jenerali Djimadoum Tiraina, makamu wa rais wa Baraza la Jeshi la Mpito, huko Ndjamena, Aprili 21, 2021. AFP - -
Matangazo ya kibiashara

Uenyekiti wa kamati hii unaongozwa na Jenerali Djimadoum Tiraina alikuwa kati ya watu waaminifu kwa Idriss Déby Itno, yeye pia ni makamu wa rais wa Baraza la Jeshi la Mpito.

Wapo pia makamu wa rais wawili: Mahamat Allahou Tahir, mwenyekiti wa chama cha Rally for Democracy and Progress. Na Jean-Bernard Padaré, mjumbe wa bodi kuu ya wabunge.

Wajumbe sita pia ni sehemu ya kamati hii. Miongoni mwao, Djimtebaye Lapia lakini pia mpinzani Célestin Topona, namba mbili wa chama cha UNDR, chama cha Saleh Kebzabo.

Kuanzishwa kwa kamati hii kunaashiria hatua mpya katika kipindi cha mpito. kamati hiyo itakuwa na jukumu la kuteua wanachama 93 wa Baraza la Mpito la Kitaifa. Wote lazima wawe na umri wa miaka 25 kulingana na amri iliyosainiwa mwishoni mwa mwezi Mei. Vyama vya kisiasa, asasi za kiraia, wanajeshi au hata vyama vya wafanyakazi. Kunlingana na duru za kidiplomasia  chaguo hilo pana litatumika kama dhamana ya mabadiliko ya amani na ya kuaminika.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.