Pata taarifa kuu
ETHIOPIA-USALAMA

Wanajeshi wa Eritrea waanza kuondoka Tigray

Ethiopia inasema wanajeshi wa Eritrea walioshiriki kwenye mapigano katika jimbo la Tigray wameanza kuondoka nchini humo wakati huu, nchi hiyo inapoendelea kupata shinikizo kutoka Jumuiya ya Kimataifa kutaka utulivu kurejea katika eneo hilo na misaada ya kibinadamu kuruhusiwa kuwafikia maelfu ya wakimbizi.

Shirika la US AID likitoa msaada wa chakula kwa wakaazi wa mji wa Adigrat, katika jimbo la Tigré.
Shirika la US AID likitoa msaada wa chakula kwa wakaazi wa mji wa Adigrat, katika jimbo la Tigré. © RFI/ Sébastien Németh
Matangazo ya kibiashara

Kuanza kuondoka kwa wanajeshi hao wa Eritrea, kumethibitishwa na Billene Seyoum, msemaji wa Waziri Mkuu Abiy Ahmed, ambaye amesema Wizara ya ulinzi imearifu kuwa wanajeshi hao wameanza kuondoka.

Ethiopia awali ilikuwa imekanusha ripoti za kuwepo kwa wanajeshi hao wa Eritrea, lakini mwezi Machi Waziri Mkuu Abiy alikiri kuwepo kwa vikosi hivyo vya kigeni na kusema kuwa vilikuwa katika mchakato wa kuanza kuondoka jimboni Tigray.

Mzozo huu wa miezi saba katika jimbo hilo, umesababisha maafa na maelfu ya wakaazi wa jimbo la Tigray kukimbia makwao, huku wanajesjhi wa Eritrea wakishtumiwa kutekeleza visa vya ukiukwaji wa haki za binadamu ikiwemo ubakaji.

Serikali ya Ethiopia, imekuwa ikishinikizwa pia kuruhusu misaada ya kibinadamu kufika katika jimbo la Tigray, huku kukiwa na ripoti kuwa inazuia misaada hiyo, madai ambayo uonggozi wa nchi hiyo umeendelea kukanusha.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.