Pata taarifa kuu
AFRIKA-AFYA

WHO: Afrika inahitaji dozi zaidi kukabiliana na COVID-19

Shirika la Afya Duniani, WHO, linasema bara la Afrika linahitaji chanjo Milioni 20 aina ya AstraZeneca ndani ya wiki sita zijazo ili kuwapa watu waliokuwa wamepata dozi ya kwanza.

Mpaka kufikia wiki hii, bara la Afrika limeshuhudia maambukizi ya watu Milioni 4.7 na wengine 130,000 wakipoteza maisha tangu kuzuka kwa maambukizi ya Corona mwaka uliopita
Mpaka kufikia wiki hii, bara la Afrika limeshuhudia maambukizi ya watu Milioni 4.7 na wengine 130,000 wakipoteza maisha tangu kuzuka kwa maambukizi ya Corona mwaka uliopita GABRIEL BOUYS AFP
Matangazo ya kibiashara

Mwakilishi wa WHO barani Afrika, Daktari Matshidiso Moeti amesema, chanjo hiyo na nyingine zinahitajika haraka ili kuokoa maisha ya watu.

Mpaka kufikia wiki hii, bara la Afrika limeshuhudia maambukizi ya watu Milioni 4.7 na wengine 130,000 wakipoteza maisha tangu kuzuka kwa maambukizi ya Corona mwaka uliopita.

Wakati huio huo Umoja wa Ulaya umeipeleka katika mahakama ya Brussels kampuni ya kutengeneza chanjo ya AstraZeneca na kuituhumu kutokuwa na nia njema katika kuyapa mataifa mengine dozi za chanjo hiyo.

Umoja wa Ulaya umeituhumu kampuni hiyo ya Uingereza na Marekani kwa kuchelewesha uuzaji wa chanjo hizo ili iihudumie Uingereza, miongoni mwa wengine.

Mkataba wa AstraZeneca iliosainiwa na Halmashauri Kuu ya Ulaya, kwa niaba ya mataifa wanachama ulihitaji kutolewa dozi za mwanzo milioni 300 kwa ajili ya kusambazwa miongoni mwa nchi 27, na chaguo la kuongeza dozi nyingine milioni 100.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.