Pata taarifa kuu
AFRIKA-USHIRIKIANO

Mkutano wa Afrika-Ufaransa wahirishwa hadi Oktoba 2021

Mkutano wa kilele kati ya Afrika na Ufaransa ambao ungelifanyika kuanzia Julai 8 hadi 10 huko Montpellier kusini mwa Ufaransa, hatimaye umeahirishwa hadi mwezi Oktoba kwa sababu ya vikwazo vya kusafiri kutokana na janga la COVID-19.

Mwaka wa 2017, mkutano wa kilele kati ya Afrika na Ufaransa ulifanyika huko Bamako, Mali. (Picha ya kumbukumbu).
Mwaka wa 2017, mkutano wa kilele kati ya Afrika na Ufaransa ulifanyika huko Bamako, Mali. (Picha ya kumbukumbu). © REUTERS/Luc Gnago
Matangazo ya kibiashara

Mgogoro wa kiafya tayari umesababisha ikulu ya Élysée kufuta mkutano kati ya viongozi wa Afrika na Ufaransa katika mji wa Bordeaux mwaka jana. Wakati huu, vizuizi vya kusafiri kutokana na kuzuka kwa janga la COVID-19 vimesababisha ikulu ya rais kuahirisha hafla hiyo.

"Vizuizi vya kusafiri vilivyowekwa kimataifa havitaondolewa vya kutosha msimu huu wa joto ili kuruhusu kuwasili kwa mamia ya wageni kutoka bara la Afrika," Halmashauri ya jiji la Montpellier limeseka katika taarifa.

Mkutano huo unaahirishwa kwa miezi mitatu. Utafanyika katika mji wa Montpellier, Oktoba 7, 8 na 9. "Tarehe hizi zinawezesha kuandaliwa kwa mkutano huu muhimu kwa nchi yetu na ukanda wetu katika mfumo mzuri," imeongeza taarifa hiyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.