Pata taarifa kuu
CHAD-SIASA

Chad: Serikali ya mpito yaidhinisha mpango wa kisiasa

Serikali ya Chad ilipitisha mpango wake wa kisiasa wakati wa kikao cha dharura cha baraza la mawaziri Jumatano, Mei 12. Rasimu ya mpango ambayo itawasilishwa Ijumaa hii kwa Bunge la nchi hiyo lililofutwa baada ya kifo cha rais Idriss Deby Itno kabla ya kurejeshwa kwa kusubiri kuchaguliwa kwa bunge la mpito.

Waziri Mkuu wa Mpito wa Chad Albert Pahimi Padacké Aprili 26, 2021 huko Ndjamena.
Waziri Mkuu wa Mpito wa Chad Albert Pahimi Padacké Aprili 26, 2021 huko Ndjamena. AFP - ISSOUF SANOGO
Matangazo ya kibiashara

Ilichukua dakika thelathini tu kwa serikali, iliyokutana katika kikao kilichoongozwa na rais wa mpito, Jenerali Mahamat Idriss Deby Itno, kudhibitisha mpango wa kisiasa wa serikali ya Albert Pahimi Padacké aliyeteuliwa Mei 2. Mpango huo unaonyesha "mwendelezo wa shughuli za Serikali, utunzaji wa amani na utulivu na kuendelea na mipango na miradi ya maendeleo" hadi mwezi Oktoba 2023. Bunge la zamani lilirejeshwa ili kuhalalisha mpango huo

Baadhi ya wizara kama vile Uchumi au Fedha zilisisitiza kufanya marekebisho wakati wa vikao. Ilikuwa ni lazima kuongeza kwenye mpango ulyopitishwa Jumatano hii, kwa mfano utambuzi wa sensa ya jumla ya raia. Mpango huo husika utawasilishwa kawaida Alhamisi hii katika Bunge kwa kujadiliwa Ijumaa.

Mnamo Mei 14, wabunge wa Bunge la zamani, walirejeshwa tena kwa kusubiri bunge la mpito, wameitishwa ili kuidhinisha mpango wa kisiasa wa serikali ya Albert Pahimi Padacké.

Wakati huo huo, wanasiasa mbalimbali na mashirika ya kiraia wanaendela na msimamo wa kuandamana dhidi ya baraza la kijeshi la mpito, ambalo wanasema bado liko mamlakani kinyume naa katiba.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.