Pata taarifa kuu
MSUMBIJI

Mradi wa gesi wa TOTAL nchini Msumbiji "hautasitishwa" moja kwa moja

Mradi wa gesi wa kampuni kutoka Ufaransa ya TOTAL nchini Msumbiji "utacheleweshwa angalau mwaka mmoja" kutokana na hali ya usalama kaskazini mwa nchi. Alisema hayo mkurugenzi anayehusika na masuala ya fedha wa kampuni hiyo ya mafuta ya Ufaransa Alhamisi Aprili 29.

Vue aérienne du méga-projet gazier d'Afungi, le 18 mars 2021.
Vue aérienne du méga-projet gazier d'Afungi, le 18 mars 2021. AFP - GRANT LEE NEUENBURG
Matangazo ya kibiashara

Jumatatu Aprili 26, kampuni ya TOTAL ilitangaza kuwa iko katika hali ngumu, hali inayosababisha kusitisha kwa muda kandarasi zinazohusiana na mradi huo wa ujenzi katika mkoa wa Cabo Delgado.

Shughuli zilizokuwa zikiendelea katika eneo hilo zilisitishwa tangu shambulio la wanajihadi katika mji jirani wa Palma Machi 24. Kulingana na Francis Perrin, mkurugenzi wa utafiti wa IRIS (Taasisi ya Uhusiano wa Kimataifa na Mkakati), mradi huo, hata kama umechelewa, hautasitishwa moja kwa moja. Uwekezaji uliofanywa ni mmkubwa mno.

"Hii ni muhimu sana kwa ukanda wa kusini mwa Afrika na kwa nchi za magharibi ambazo zinaunga mkono Msumbiji. Kwa hivyo kuna faida kubwa kwa mradi huu - faid za kiuchumi bila shaka, faida za kifedha, faida za kijiografia - ambayo nadhani mradi huu utafanywa. Swali ni kuhusu kalenda ya mradi huu, ambao kwa kawaida ungeingia katika hatua ya uzalishaji mnamo mwaka 2024 ", amesema Francis Perrin.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.