Pata taarifa kuu
UFARANSA

Ufaransa: Afisa wa polisi auawa kwa shambulio la kisu Rambouillet

Mtu mmoja alimdunga kisu afisa wa polisi mwanamke katika kituo cha polisi cha Rambouillet, kilomita 60 kutoka mji mkuu wa Ufaransa, Paris, kabla ya kuuawa kwa kupigwa risasi. Ofisi ya mashtaka inayopambana na ugaidi imeanzisha uchunguzi.

Eneo alikouawa afisa wa polisi mmwanamke baada ya kushambuliwa kwa kisu na mtu mmoja katika kituo cha polisi cha Rambouille, Ufaransa.
Eneo alikouawa afisa wa polisi mmwanamke baada ya kushambuliwa kwa kisu na mtu mmoja katika kituo cha polisi cha Rambouille, Ufaransa. Bertrand Guay AFP
Matangazo ya kibiashara

Tukio hilo limetokea karibu saa 8:20 mchana kwenye katika kituo cha polisi cha Rambouillet. Mwanamume mmoja alimdunga kisu  afisa wa polisi kwenye koo mara mbili alipokuwa akienda nyumbani kwa mapumziko ya chakula cha mchana. Chanzo cha polisi kinabaini kwamba muuaji alisema "Allah Akhbar" wakati wa kutekeleza uahlifu wake. Lakini alipigwa risasi na afisa mwingine wa polisi na kufariki dunia papo hapo.

Afisa huyo mwanamke aliyeuawa kwa shambulio la kisu alikua na umri wa miaka 49, na alikuwa afisa wa utawala wa sekretarieti ya kituo cha polisi cha Rambouillet. Afisa hyo wa polisi alikuwa mama wa watoto wawili, wa miaka 13 na 18.

Kitendo cha kinyama kwa shujaa wa kila siku

Mshambuliaji ni raia wa Tunisia mwenye umri wa miaka 36 ambaye aliwasili nchini Ufaransa mwaka 2009, akiingia kinyume cha sheria na tangu wakati huo aliishi nchini Ufaransa kwa vyeti halali. Hakujulikana na polisi na idara ya ujasusi, vyanzo kadhaa vya polisi vimethibitisha kwa shirika la habari la AFP. Kulingana na chanzo kilicho karibu na uchunguzi, alikuwa amehamia katika eneo la Rambouillet.

Waziri Mkuu Jean Castex na Waziri wa Mambo ya Ndani Gérald Darmanin wamezuru eneo la tukio. Katika ujumbe uliotumwa kwenye Twitter, kiongozi wa serikali ameshutumu "kitendo cha kinyama" dhidi ya "shujaa wa kila siku".

"Hatutokubali kushindwa" kwa "ugaidi wa wa wanamgambo wa Kiislam," amesema Emmanuel Macron kwenye ukurasa wake wa Twitter.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.