Pata taarifa kuu
SUDAN

UN: Mapigano ya kikabila Darfur Magharibi yamesababisha vifo vya watu 40

Takriban watu 40 wameuawa na 58 wamejeruhiwa katika mapigano ya kikabila tangu Jumamosi (Aprili 3) huko El-Geneina, mji mkuu wa Darfur Magharibi, ghasia mbaya za hivi karibuni hadi sasa katika eneo hili linalokabiliwa na machafuko magharibi mwa Sudan, Umoja wa Mataifa umesema.

Mwezi Januari, watu 129 waliuawa na wanajeshi zaidi waliltumwa katika eneo la El Geneina. Hata hivyo, kulingana na vyanzo vya ndani, vikosi hivi vimejiondoa tangu wakati huo.
Mwezi Januari, watu 129 waliuawa na wanajeshi zaidi waliltumwa katika eneo la El Geneina. Hata hivyo, kulingana na vyanzo vya ndani, vikosi hivi vimejiondoa tangu wakati huo. Ashraf Shazly AFP/Archivos
Matangazo ya kibiashara

“Tangu Aprili 3, watu 40 wameuawa katika mapigano ya hivi karibuni kati ya jamii ya Massalit na makabila ya Kiarabu. Hali inaendelea kuwa ya wasiwasi katika mji wa Al Geneina, ”Ofisi ya Umoja wa Mataifa inayohusika na uratibu wa misaada ya kibinadamu (OCHA) imesema katika taarifa. "Tume ya misaada ya kibinadamu ya serikali inaripoti [...] watu 58 wamejeruhiwa," imeongeza.

Milio ya risasi ilisikika katika mji huo siku ya Jumatatu, huku watu wakionekena kutoroka makaazi yao wakihofia usalama wao.

Hali ni ya wasiwasi katika mji huo na tayari serikali imetangaza hali ya hatari katika eneo la Magharibi mwa jimbo la Darfur.

Jimbo la Darfur tangu mwaka 2003 limekosa utulivu, mapigano ya wenyewe kwa wenyewe, yamesababisha vifo vya watu zaidi ya Laki tatu na wengine Milioni 2.5 kuyakimbia makwao kwa mujibu wa takwimu za Umoja wa Mataifa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.