Msumbiji: TOTAL yahamisha wafanyakazi wake baada ya shambulio la IS
Kampuni ya Ufaransa ya mafuta ya TOTAL imeamua kuhamisha wafanyakazi wake wote kutoka katika eneo linakofanyia shughuli zake za uchimbaji wa gesi kutokana na uwezekano wa kutokea mashambulizi zaidi ya kigaidi katika mkoa wa mji wa Palma, nchini Msumbiji.
Imechapishwa:
Kampuni ya TOTAL imeamua kuondoa wafanyakazi wote kutoka eneo lake la gesi kaskazini mashariki mwa Msumbiji, siku tisa baada ya shambulio la wanajihadi katika mji jirani wa Palma, na mradi wa mabilioni ya euro umesimama moja kwa moja tangu Ijumaa wiki hii.
Machi 24, kundi lenye silaha lilishambulia mji Palma, wenye wakaazi 75,000, na kuua raia wengi, ikiwa ni pamoja na maafisa wa polisi na wanajeshi. Shambulizi hilo lililoandaliwa kwa uangalifu, ambalo lilitekelezwa kilomita chache tu kutoka eneo kunakoendeshwa mradi mkubwa wa gesi kwenye rasi ya Afungi, lilidaiwa na kundi la Islamic State (IS).
“Total imechukua uamuzi wa kuwaondoa wafanyakazi wote. Kwa wakati huu, mitambo yote imeachwa bila ulinzi, "chanzo cha jeshi kimeliambia shirika la habari la AFP. "TOTAL imewahamisha wafanyakazi wake," kimethibitisha chanzo cha usalama. Waasi wameonekana katika siku za hivi karibuni karibu na eneo hilo la TOTAL, kulingana na chanzo cha usalama. Maelfu ya watu waliotoroka mji wa Palma kwa muda wa siku tisa wamekuwa wakikimbilia kwenye eneo hilola Afungi kunakoendeshwa mradi huo wa uchimbaji gesi.