Pata taarifa kuu
COTE D'IVOIRE

Raia wa Cote d'Ivoire washerehekea kuachiliwa huru kwa Gbagbo na Blé Goudé

Laurent Gbagbo na Charles Blé Goudé waliachiliwa huru. Mahakama ya Rufaa ya ICC ilitoa uamuzi wake Jumatano hii alasiri, Machi 31, huko Hague. Habari hii ilikuwa ikisubiriwa kwa hamu na wanaharakati na wafuasi wa chama cha FPI, chama cha Gbagbo, hatua ambayo wafuasi hao wamepongeza.

Wafuasi wa rais wa zamani Laurent Gbagbo wanasherehekea tangazo la kuachiliwa huru kiongozi huyo wa zamani, Machi 31, 2021.
Wafuasi wa rais wa zamani Laurent Gbagbo wanasherehekea tangazo la kuachiliwa huru kiongozi huyo wa zamani, Machi 31, 2021. AFP - SIA KAMBOU
Matangazo ya kibiashara

Laurent Gbagbo na Charles Blé Goudé waliachiliwa huru. Mahakama ya Rufaa ya ICC ilitoa uamuzi wake Jumatano hii alasiri, Machi 31, huko Hague. Habari hii ilikuwa ikisubiriwa kwa hamu na wanaharakati na wafuasi wa chama cha FPI, chama cha Gbagbo, hatua ambayo wafuasi hao wamepongeza.

Katika wilaya ya Selmer ya Yopougon ambapo mwandishi wetu Sidy Yansané alitembelea, wafuasi wa Gbagbo na waziri wake wa zamani Blé Goudé wamesema wameshinda kesi ambayo ilichukua muda mrefu na hivyo wana imani ya kuomuona kiongozi wao anarudi nchini Cote d'Ivoire.

Kesi ya rais wa zamani wa Cote d'Ivoire na waziri wake wa zamani Charles Blé Goudé ilianza mwezi Januari 2016. Wote wawili waliachiliwa huru katika kitengoch kwanza cha mahakama hiyo, mwanzoni mwa mwaka 2019, baada ya kushtumiwa uhalifu dhidi ya binadamu na uhalifu wa kivita, katika muktadha wa vurugu zilizofanywa kati ya Desemba 2010 na Aprili 2011, kufuatia kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi wa urais. ICC inatarajia kutoa uamuzi juu ya kuachiliwa kwao huru leo Jumatano.

Kwa upande wa Mwendesha mashitaka mkuu wa ICC Fatou Bensouda, wengi wanaona kuwa ni pigo jingine baada ya kushindwa kuonyesha ushahidi wa kutosha kwa kuhusika kwa Laurent Gbagbo na Charles Blé Goudé katika machafuko hayo ya baada ya uchaguzi nchini Cote d'Ivoire ambayo yalisababisha vifo vya watu wengi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.