Pata taarifa kuu
MSUMBIJI

Ureno kusaidia kijeshi Msumbiji baada ya shambulio la kigaidi

Ureno imesema inatarajia kuwapeleka wanajeshi wake nchini Mdsumbiji kusaidi jeshi la nchi hiyo linalokabiliana na wanamgambo wa Kiislamu, baada ya mashambulio dhidi ya mji wa Kaskazini mwa nchi hiyo ambayo yamesababidha vifo vingi na maelfu ya raia kuyahama makaazi yao.

Mji wa Palma uko kaskazini mashariki mwa Msumbiji.
Mji wa Palma uko kaskazini mashariki mwa Msumbiji. © RFI
Matangazo ya kibiashara

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ureno Augusto Santos Silva amesema karibu askari 60 wanajiandaa kuelekea Msumbiji kuyapa usaidizi majeshi ya nchi hiyo.

IS yadai kudhibiti Palma, Kaskazini mwa Msumbiji

Wakati huo huo Kundi la Islamic State limedai kuhusika na shambulio la Palma, katika mkoa wa Cabo Delgado, kaskazini mwa Msumbiji.

Shambulio ambalo, kulingana na mamlaka huko Maputo, limeua watu kadhaa na kusababisha maelfu ya raia kuyatoroka makaazi yao tangu Jumatano wiki iliyopita.

Kundi la kijihadi ambalo kundi la wanamgambo wa Kiislamu nchini Msumbiji la Ansar al-Sunna limejiunga, linadai "kudhibiti mji wa pwani", kilomita chache kutoka eneo kunakoendeshwa mradi wa mkubwa wa gesi wa kampuni ya Ufaransa ya TOTAL, mradi ambao umesitishwa tena tangu Jumamosi wiki iliyopita.

Kulingana na taarifa kutoka kundi la Islamic State, wanajihadi wamedhibiti mji wa Palma baada ya siku tatu za mapigano. Waliua wanajeshi 55 na "Wakristo" au raia kutoka nchi za Magharibi, na kuharibu majengo ya serikali na benki.

Kwa upande wao, vikosi vya Msumbiji vinakadiria idadi ya watu waliouawa kwa makumi kadhaa na wanasema wameanzisha tena mapigano kwa lengo la kurejesha kwenye himaya yao mji huo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.