Pata taarifa kuu
CAR-UN-SIASA-USALAMA

Ripoti ya Guterres: Jamhuri ya Afrika ya Kati "iko katika hatua ya kuchukuliwa maamuzi"

Ripoti mpya ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Atonio Guterres kuhusu Jamhuri ya Afrika ya Kati imetangazwa kwa umma.

Waziri Mkuu Firmin Ngrebada akitembelea wanajeshi wa serikali wanaowakabiliana na waasihuko Boali Jumapili hii, Januari 10, 2021.
Waziri Mkuu Firmin Ngrebada akitembelea wanajeshi wa serikali wanaowakabiliana na waasihuko Boali Jumapili hii, Januari 10, 2021. © Charlotte Cosset/RFI
Matangazo ya kibiashara

Katibu Mkuu wa Umoja wa MAtaifa ameelezea matukio mbalimali yaliyotokea tangu Oktoba 12 na amezugumzia kipindi cha kabla na baada ya uchaguzi.

Jamhuri ya Afrika ya KAti ilikabiliwa na machafuko yaliyoogezeka kwa kasi wakati wa uchaguzi na kuundwa kwa muugano mpya wa waasi ambao uliendesha mashambulizi kuelekea mji mkuu wa nchi hiyo Bangui na kuvuruga uchaguzi.

Katibu mkuu anaona katika matamshi yake kuwa ilikuwa "muhimu" uchaguzi ufanyike "katika muda uliowekwa kikatiba". Na kuhakikisha kwamba "Jamhuri ya Afrika ya Kati iko katika hatua ya maamuzi".

"Ghasia za uchaguzi zilisababisha ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu," ripoti inasema.

Inabainisha ongezeko la zaidi ya asilimia 60 ya ukiukaji wa haki za binadamu kati ya mwezi Oktoba 2020 na mwezi Februari 2021.

Visa hivi vya ukiukaji vilitekelezwa na makundi yenye silaha lakini pia vikosi vya serikali, ikiwa ni pamoja na ututekelezwaji wa sheria ya kutotoka nje iliyowekwa nchi nzima ambayo ilisababisha matumizi ya nguvu za kupita kiasi”.

Kulingana na ripoti ya Umoja wa Mataifa, "Askari wa kikosi cha Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati (MINUSCA) waliweza kuingilia kati katika hali hiyo, kwani shinikizo kwa tume ya umoja huo ilizidi vikosi vya usalama vya kitaifa kuanza kutoroka na wengine kuasi ." Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa ameomba "kuimarisha utawala wa sekta ya usalama" na "mchakato mzuri wa mageuzi".

Kupelekwa kwa wanajeshi chini ya makubaliano ya pande mbili kuliwezesha kukabiliana na hali hiyo, amekiri katibu mkuu - bila kutaja Urusi au Rwanda. Walakini, ametoa wito wa uratibu mzuri kati ya washirika wanaosimamia usalama "ili kuhakikisha ulinzi wa walinda amani na kuwezesha misaada ya kibinadamu inawafikia walengwa.

Ripoti hiyo imeelezea mgogoro wa kibinadamu unaozidi kuwa mbaya. Zaidi ya nusu ya raia wa nchi hiyo wanahitaji msaada wa kibinadamu leo. Matukio dhidi ya mashirika ya kutoa misaada yanaongezeka. Mnamo mwezi Januari 2021: Matukio 66 yalirekodiwa, idadi kubwa zaidi kuwahi kurekodiwa. Mnamo mwaka wa 2020, matukio 424 yalitokea na kusababisha vifo 3 na majeruhi 29. Tangu katikati ya mwezi Desemba, watu zaidi ya 240,000 wamehama makazi yao "kwa sababu ya vurugu zinazohusiana na uchaguzi". Nusu ya hawa waliotoroka makaazi yao bado hawajaweza kurudi nyumbani.

 

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.