Pata taarifa kuu
DRC- USALAMA

Waasi wa FDLR-FOCA, watuhumiwa kwa mauaji ya Balozi wa Italia

Serikali nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imewashtumu waasi wa FDLR wenye asili ya Rwanda, kwa kumshambulia na kumuua balozi wa Italia nchini humo Luca Attanasio hapo jana karibu na mji wa Goma, mashariki mwa nchi hiyo.

Sehemu ya wapiganaji wa kundi la FDLR ambalo limesema wapiganaji wake wataendelea kujisalimisha
Sehemu ya wapiganaji wa kundi la FDLR ambalo limesema wapiganaji wake wataendelea kujisalimisha Reuters
Matangazo ya kibiashara

Balozi Attanasio alikuwa katika msafara wa Shirika la mpango wa chakula duniani WFP wakati gari lao liliposhambuliwa.

Hata hivyo, kundi la FDLR limekanusha kuhusika na shambulizi hilo, kwa kile inachosema vikosi vyake viko mbali na eneo la shambulizi hilo.

Maafisa katika mbuga ya wanyamapori ya Virunga wanasema shambulio hilo lilikuwa jaribio la utekaji nyara lililoshindikana, pale walipoingilia kati mara moja.

Makundi mengi ya wapiganaji wenye silaha yameendelea kujiimarisha ndani na pembezoni mwa mbuga hiyo inayopakana na nchi jirani za Rwanda na Uganda.

Waziri wa mambo ya nje wa jamhuri wa DRC Marie Ntumba Nzeza amefahamisha kuwa serikali yake imeanzisha uchunguzi kubaini wahusika wa mauaji hayo na kwamba mpaka sasa hawajakamatwa.

Mbali na balozi huyo wa Italia kuuawa, dereva wa gari raia wa Congo pia aliuawa katika tukio hilo. 

 

 

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.