Pata taarifa kuu
DRC- USALAMA

Balozi wa Italia auawa mashariki mwa DRC

Balozi wa Italia nchini Jamhuri ya Demokrasia ya Congo, Luca Attanasio, ameuawa, baada ya msafara wao kushambuliwa, taarifa kutoka wizara ya mambo ya nje ya Italia imethibitisha.

Wanajeshi wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa wakipiga doria, hapa ni katika hifadhi ya taifa ya wanyama ya Virunga, Desemba mwaka 2013.
Wanajeshi wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa wakipiga doria, hapa ni katika hifadhi ya taifa ya wanyama ya Virunga, Desemba mwaka 2013. REUTERS/Kenny Katombe
Matangazo ya kibiashara

Kisa hicho kimetokea karibu na mji wa Kanyamahoro mapema jumatatu, mashariki mwa DRC, kikihusishwa na watekaji ambao walikuwa wakiuvizia msafara huo.

Gavana wa mkowa wa Kivu Kaskazini, Carly Nzanzu Kasivita, ameliambia shirika la habari la Ufaransa, kuwa balozi huyo alikuwa miongoni mwa msafara wa shirikala umoja wa mataifa la mpango wa chakula WFP, wakiwa wanatembelea nje kidogo ya jiji kuu la Goma kutathimini hali ya usalama katika eneo hilo la mashariki mwa jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Maafisa wa usalama wa mbunga ya wanyama pori ya Virunga, wamethibitisha kuwa balozi Luca Attanasio, ameuawa pamoja na mlinzi wake.

Makundi mengi ya waasi yamekuwa yakiendesha shughuli zake mashariki mwa DRC, hasa eneo ambalo lipo karibu na mpaka wa mataifa ya Rwanda na Uganda.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.