Pata taarifa kuu
DRC-UN

UN yasikitishwa na mwendelezo wa mauaji ya raia nchini DRC

Umoja wa Mataifa umesema zaidi ya raia 2,000 waliuuawa mwaka 2020 katika mikoa mitatu Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia Congo, wakati huu watu wengine 10 wakiuawa katika mauaji ya hivi punde, Wilayani Beni.

Hasara iliyosababishwa na waasi wa ADF baada ya kutekeleza shambulizi wilayani Beni Mashariki mwa DRC katika siku za hivi karibuni
Hasara iliyosababishwa na waasi wa ADF baada ya kutekeleza shambulizi wilayani Beni Mashariki mwa DRC katika siku za hivi karibuni John WESSELS / AFP
Matangazo ya kibiashara

Takwimu hizi za Umoja wa Mataifa zimetolewa wakati huu mashambulizi dhidi ya raia yakiendelea katika maeneo mbalimbali ya Mashariki mwa nchi hiyo hasa Wilayani Beni.

Babar Baloch Msemaji wa Tume ya Umoja inayoshughuikia wakimbizi UNHCR, amesema raia Mashariki mwa nchiu hiyo wanaendelea kuishi kwa woga kufuatia mwendelezo wa mashambulizi kutoka kwa makundi ya waasi.

Mwaka 2020 pekee; watu 1,240 waliuawa mkoani Ituri, 590 Kivu Kaskazini na wengine 261 Kivu Kusini.

Aidha, Umoja wa Mataifa umeainiani kuwa mashambulizi hyao yameendelea kuwalenga wakimbizi waliokimbia makwao mwaka huu wa 2021 wakati huu kukiwa na wakimbizi zaidi ya Elfu 88.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.