Pata taarifa kuu
DRC-SIASA

Bunge la kitaifa lamtimua Waziri Mkuu Sylvestre Ilunga

Bunge la kitaifa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia limeamua kumtimua Waziri Mkuu Sylvestre Ilunga baada ya kupiga kura ya kutokuwa na imani naye Jumatano wiki hii.

Félix Tshisekedi (Kulia) Waziri Mkuu Sylvestre Ilunga Ilunkamba aliyepigiwa kura ya kukosa imani naye
Félix Tshisekedi (Kulia) Waziri Mkuu Sylvestre Ilunga Ilunkamba aliyepigiwa kura ya kukosa imani naye Présidence de la République démocratique du Congo
Matangazo ya kibiashara

Sylvestre Ilunga ni mshirika wa karibu wa rais wa zamani Joseph Kabila.

Kutimuliwa kwake kumepelekea ushindi wa kisiasa kwa rais wa sasa wa nchi hiyo Felix-Antoine Tshisekedi, ambaye hivi karibuni alitangaza kuvunja muungano wa kisiasa uliokuwa ukijumuisha muungano wa FCC wa Joseph Kabila na muungano wa CASH.

Sylvestre Ilukamba, ambaye hakuwepo wakati wa kura ya kutokuwa na imani naye iliyopigwa bungeni, amepewa saa 24 ili awe amejiuzulu.

Wabunge wanamshutumu Sylvestre Ilunga na mawaziri wake kwa utendaji kazi mbovu.

Kura ya kutokuwa na imani naye ilipitishwa na wabunge wengi: kura 367 zilipigwa kwa jumla ya wabunge 377 walioshiriki kiako cha Jumatano.

Kwa upande wa wabunge wanaotetea uamuzi wa kumuangusha Bw. Ilunga, wanasema serikali ya Sylvestre Ilunga "haikuwajibika kwa utendaji kazi wake", "haikutimiza ahadi zake", kwa mfano katika sekta ya usalama.

Wabunge hawa wametaja pia "mauaji ambayo yanaendelea mashariki mwa nchi", uwepo wa majeshi ya kigeni katika ardhi ya Congo na ukosefu wa usalama katika baadhi ya miji ya nchi hiyo.

Wabunge hawa wameshtumu ukosefu wa utawala wa haki na ufisadi.

Kuanguka kwa serikali kunafungua milango kwa Rais Félix Tshisekedi kuteua mawaziri watiifu kwake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.