Pata taarifa kuu
ETHIOPIA

Serikali yaendelea kuwasaka viongozi wa Chama TPLF

Katika jimbo la Tigray, ambapo serikali kuu ya Addis Ababa haijaweza kudhibiti baadhi ya maeneo, hali bado ni tete, kulingana na maoni kutoka kwa mashirika ya kutoa misaada na vyanzo vya kiusalama.

Jeshi la Ethiopia
Jeshi la Ethiopia REUTERS/Tiksa Negeri/File Photo
Matangazo ya kibiashara

Kufikia sasa bado viongozi wa chama kilichoasi cha TPLF, ambao wanaendelea kusakwa na mamlaka, hawajaweza kupatikana, hata kama baadhi yao wamekamatwa na wengine kuuawa.

Vikosi vya serikali ya Addis Ababa havikusumbuka kwa kulidhibiti jimbo la Tigray.

Spika wa zamani wa Bunge Keria Ibrahim alikuwa nyumbani kwake Mekele na alijisalimisha kwa hiari yake mnamo Novemba 30 wakati jeshi la shirikisho lilipoingia. Sababu za kiongozi huyo kutokimbilia mafichoni zinajulikana: alikuwa mjamzito, vyanzo kutoka idara ya usalama vimebaini.

Katikati mwa operesheni ya jeshi, jeshi lilichapisha majina ya viongozi wa chama cha TPLF wanaodaiwa kuwa walikamatwa milimani. Miongoni mwao, mfanyabiashara mzee Sebhat Nega, mwanzilishi mwenza wa chama hicho na bado anachukuliwa kama kiongozi wa kiroho wa chama hicho, alikamatwa Januari 8 na dada yake, mkewe na maafisa kadhaa.

Na siku iliyofuata Balozi Abay Woldu, rais wa zamani wa mkoa huo, lakini pia Waziri wa zamani wa Fedha Abraham Tekeste walikamatwa. Wote walifikishwa katika mahakama ya Addis Ababa mnamo Januari 15.

Viongozi wengine maarufu waliuawa mwezi huu katika mazingira tatanishi, pamoja na waziri wa zamani wa mambo ya nje wa Ethiopia Seyoum Mesfin.

Mamlaka huko Addis Ababa bado inawasaka viongozi wengine sitini wa chama cha TPLF, ikiwa ni pamoja na kiongozi wa cham hicho, Debretsion Ghebremichael, na mshauri wake maalum, Waziri wa zamani wa Mawasiliano Getachew Reda.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.