Pata taarifa kuu
JAMHURI YA AFRIKA YA KATI

Ripoti ya Umoja wa Mataifa kuhusu nchi ya Jamhuri ya Afrika ya Kati

Jopo la wataalam la Umoja wa Mataifa lililopewa jukumu la kuchunguza visa vya ukiukaji wa wa vikwazo vya silaha nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati liliwasilisha ripoti yake ya awali ya mwaka huko New York mnamo Alhamisi, Januari 21.

Wajumbe wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa wakipiga kura.
Wajumbe wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa wakipiga kura. UN Photo/Loey Felipe
Matangazo ya kibiashara

Hata hivyo ripoti hiyo itawekwa waz mwishoni mwa mwezi huu, lakini RFI imeweza kupata kopi ya ripoti hiyo na na habpa inaeleza baadhi ya vipengele vya ripoti yenyewe.

Uchunguzi uliomo katika ripoti ulifanywa kwa sehemu kubwa kabla ya uchaguzi wa mwezi Desemba na kabla ya kuundwa kwa muungano wa waasi nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, CPC, ambao leo unatishia utawala wa Bangui.

Wataalam, hata hivyo, wanamhusisha rais wa zamani François Bozizé, ambaye anakabiliwa na vikwazo vya Umoja wa Mataifa, katika uundwaji wa muungano huo wa waas.

Kuhusu usafirishaji wa silaha nchini -uamuzi uliyoidhinishwa chini ya baadhi ya masharti- wataalam wanakumbusha wanajeshi wa Jaùhuri ya Afrika ya Kati jukumu lao la kuhakikisha ulinzi na ufuatiliaji wa vifaa vyao.

Wanasema kuwa vifaa vya kijeshi ambavyo viliwasili mwezi Oktoba mwaka jana huko Bangui kutoka Urusi havikusajiliwa na serikali ya Jamuhuri ya Afrika ya Kati mwezi Desemba, na wanasema wana ushahidi kwamba vifaa hivi viliishia mikononi mwa washirika wa muungano wa makundi ya waasi ya CPC, 3R na anti-balaka hasa, mwishoni mwa mwezi Desemba huko Boali.

Wataalam pia wanasema kwamba "taarifa" za uwasilishaji silaha ambazo nchi husika huwasilisha kwa kamati ya vikwazo zina mashaka, na hivyo kuwa ngumu kutekeleza marufuku hiyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.