Rais Chakwera atangaza hali ya dharura kukabili janga la Corona
Rais wa Malawi Lazarus Chakwera ametangaza hali ya hatari kutokana na ongezeko la maambukizi ya virusi vya corona nchini humo ambayo yamefikia zaidia ya Elfu tisa na vifo zaidi ya mia mbili.
Imechapishwa:
Mbali na ongezeko hilo, hatua hii inakuja baada ya Mawaziri wake wawili kufariki dunia kutokana na virusi hivyo.
“Kila mmoja wetu lazima aijali afya ya mwingine na kila mmoja wetu lazima avae barakoa hadharani lazima aoshe mikono kabla na baada ya shughuli yoyote,”.
“Lazima tuweke umbali na wengine ili kuepuka maambukizi,na tuondoke kwenye maeneo yakiyojazana watu maana hakuna mmoja wetu yupo salama kwa hiyo inamaanisha kila mmoja wetu lazima awajibike, amesema.
Maombolezo ya kitaufa ya siku tatu yametangzwa nchini humo kuwakumbuka watu waliopoteza maisha.