Pata taarifa kuu
CHAD

Chad: Kiongozi wa zamani wa upinzani Saleh Kebzabo akabiliwa na mashitaka

Mbunge na kiongozi wa zamani wa upinzani nchini Chad, Saleh Kebzabo, anakabiliwa na hatari ya kuchukuliwa hatua za kisheria, kulingana na barua kutoka kwa waziri wa Sheria iliyowasilishwa bungeni, ambayo RFI imepata nyaraka.

Saleh Kebzabo mwanasiasa wa upinzani nchini Chad
Saleh Kebzabo mwanasiasa wa upinzani nchini Chad RFI/Christophe Boisbouvier
Matangazo ya kibiashara

Kulingana na waraka huo, mpinzani huyo anadaiwa kuwa alitoa matamshi ya kuchochea chuki na kuhatarisha usalama wakati aliomba vijana wakulima wakati wa mkutano wa kisiasa kujipanga kulinda mashamba yao dhidi ya wafugaji.

Saleh Kebzabo alikutwa na hatia ya matamshi Desemba 22 mwaka uliopita yanayoweza kuhatarisha amani na utulivu wa umma.

Hayo yamo katika barua iliyosainiwa na waziri wa Sheria wa Chad Desemba 28 na kupelekwa kwa spika wa Bunge.

Ikiwa barua ya Waziri wa Sheria itaidhinishwa na wabunge, utaratibu wa kugfungua mashitaka utazinduliwa dhidi ya kiongozi wa zamani wa upinzani lakini bila uhakika wowote wa kujuwa iwapo hatua za kisheria zitachukuliwa.

Saleh Kebzabo anashutumiwa ni kuzuru mkoa wa Tandjile Desemba 22, ambapo kulitokea mapigano kati ya wakulima na wafugaji baada ya uharibifu wa shamba.

Maneno yake yalionekana kuwa yalihatarisha amani na utulivu wa umma.

Kiongozi huyo wa zamani wa upinzani aliwahimiza vijana kutafuta uwezo wa kulinda mashamba ya wazazi wao kutokana na uzembe wa viongozi. Maneno ambayo yalionekana na serikali kuwa ni hatari kwa amani.

Mapigano kati ya wakulima yameongezeka katika miaka ya hivi karibuni, ikionyesha zaidi udhaifu wa utawala kutokuwa na uwezo wa kutatua mizozo inayohusiana na umiliki wa maliasili.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.