Pata taarifa kuu
UFARANSA-MISRI-DIPLOMASIA

Rais wa Misri nchini Ufaransa: Ziara ya Serikali yenye changamoto nyingi

Rais wa Misri Abdel Fattah al-Sisi yuko nchini Ufaransa tangu Jumapili hii, Desemba 6 kwa ziara ya kiserikali ya siku mbili inayolenga kuimarisha ushirikiano kati ya Ufaransa na Misri wakati mgogoro unaendelea kushuhudiwa Mashariki ya Kati.

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron akiwa na rais wa Misri walipokutana mwaka 2017 jijini Paris
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron akiwa na rais wa Misri walipokutana mwaka 2017 jijini Paris AP
Matangazo ya kibiashara

Katika ziara hiyo pia itakuwa swali la kufufua uhusiano wa pande mbili uliingiliwa dosari na suala la haki za binadamu.

Kwa upande wa Elysee, Misri ya Marshal al-Sisi ni moja wapo ya nchi zenye utulivu " katika ukanda" huo ambao uko hatarini".

Duru kutoka vyanzo vya kuaminika vilivyo karibu na wasaidizi wa rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, vinabaini Ufaransa inasisitiza juu ya umuhimu wa "kuimarisha ushirikiano wa kimkakati" kati ya Cairo na Paris.

Misimamo ya marais hao wawili inatofautiana katika maswala makubwa ya kiusalama ya ukanda wa Mashariki ya Kati: mzozo kati ya Israeli na nchi za Kiarabu, mzozo wa kisiasa nchini Lebanon, maswala yanayohusiana na Iran pamoja na Iraq lakini pia malengo ya rais wa Uturuki Recep Tayip Erdogan katika Bahari ya Mashariki.

Uturuki inataka, kwa kutumia nguvu za kijeshi, kukabiliana na Ugiriki kwa kulidhibiti eneo hilo lenye utajiri wa gesi. Athenes, ambayo inaungwa mkono na Paris, imejiunga kijeshi na Misri, ambapo jeshi lake la majini sasa linaweza kushindana na Uturuki baada ya kupokea meli kutoka Ufaransa.

Marais hao wawili pia wanapingana na rais Erdogan kuhusu mzozo wa Libya. Ikiwa rais wa Uturuki anaunga mkono kijeshi na kifedha serikali ya Tripoli, Misri na Ufaransa wanamuunga mkono mpinzani wake, Marshal Haftar.

Marshal al-Sisi pia anaonesha Misri kama kizuizi dhidi ya wahamiaji haramu wanaokwenda Ulaya, bila kusahau jukumu lake kama kinga dhidi ya Uislamu wa kisiasa katika Mashariki ya Kati, wakati Rais Macron ameanza kushambulia kundi la Muslim Brotherhood kama maadui wakumbwa wa Marshal al-Sisi.

Hata hivyo rais al-Sisi amekuwa akikosolewa kukandamiza maandamano ya wapinzani wake na kuvunja haki za binadamu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.