Pata taarifa kuu
ETHIOPIA-ABIY AHMED

Ethiopia: Hali ya wasiwasi yaendelea kutanda katika mji wa Mekele

Habari mbalimbali zimeanza kuvuja baada ya vikosi vya serikali kuu ya Ethiopia kudai kwamba wameudhibiti mji mkuu wa Tigray, Mekele, Jumamosi, Novemba 28.

Wanajeshi wa eneo la Amhara, wakirejea kwenye kambi yao ya Danasha, baada ya kukabiliana na wapiganaji wa Tigray
Wanajeshi wa eneo la Amhara, wakirejea kwenye kambi yao ya Danasha, baada ya kukabiliana na wapiganaji wa Tigray Tiksa Negeri/Reuters
Matangazo ya kibiashara

Shirika la Msalaba Mwekundu linasema kwamba hospitali za jiji zimezidiwa na idadi ya majeruhi na zinakabiliwa na uhaba wa vifaa vya matibabu na chakula.

Wakati huo huo, kila upande umeendelea kudai kudhibiti maeneo kadhaa katika jimbo la Tigray, bila hata hivyo kuweza kuzithibitisha.

Jumapili, Novemba 29 hali ya utulivu iliripotiwa huko Mekele, kulingana na Shirika la Msalaba Mwekundu. Shirika la Msalaba Mwekundu pia limewataja Waeritrea wengi, ambao waliwasili Jumamosi katika mji huo wakiwa na njaa, baada ya kutembea kutoka kambi ambazo walikuwa wakiishi karibu na mji wa Shire.

Kwa upande wao, makamanda wa jeshi la shirikisho wameendelea kutoa taarifa juu ya hali hiyo, na hasa juu ya tishio la mashambulizikutoka vikosi vya TPLF baada ya kuingia msituni. Na huko Humera, kwenye mpaka na Sudan, televisheni ya serikali imeripoti kwamba jeshi limegundua makaburi 70 na makaburi ya halaki katika eneo la uwanja wa ndege.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.