Pata taarifa kuu
CAR-S

Michel Djotodia: Sintowania katika uchaguzi wa urais wa Desemba 21

Rais wa zamani wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, Michel Djotodia, ametoa msimamo wake katika Uchaguzi Mkuu wa Desemba 21, akibaini kwamba hatowania katika uchaguzi huo kwenye kiti cha urais kutokana na kuwa hatimizi masharti ya kuwa mgombea katika uchaguzi huo.

Rais wa zamani wa Afrika ya Kati Michel Djotodia, aliporejea Bangui, Januari 10, 2020.
Rais wa zamani wa Afrika ya Kati Michel Djotodia, aliporejea Bangui, Januari 10, 2020. FLORENT VERGNES / AFP
Matangazo ya kibiashara

Rais huyo wa zamani aliyechukuwa madaraka kupitia mtutu wa bunduki mwaka 2103 ametoa wito wa kuheshimu sheria na kuacha demokrasia kuendelea kukita mizizi nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Djotodia alirudi nchini mwaka huu baada ya miaka sita akiwa ukimbizini kufuatia makubaliano ya kisiasa ya amani na maridhiano na kufuatia sheria inayohusiana na hadhi ya wakuu wa nchi wa zamani.

Katika hotuba yake, ambayo imekuwa ni gumzo katika mji mkuu wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, Bangui, juu ya uwezekano wa François Bozize kuwania katika kinyang'anyiro hicho, ametoa wito wa kuhesimu sheria.

"Nimeamua kutowania katikaa uchaguzi ujao wa uraiswa Desemba 21, 2020, kwani sikidhi masharti yote ya yanayohitajika.Kwa upande wangu, ningependa kuwatakia mafanikio mema, kuanzia sasa, kwa wananchi wenzangu watakaochaguliwa kwa uchaguzi ujao. Walakini, wale wenzangu ambao watakuwa katika hali sawa na mimi, kama wanademokrasia wazuri, tuna jukumu la kuheshimu sheria za nchi yetu.Nchi yetu, Jamhuri ya Afrika ya Kati , " amesema Michel Djotodia.

"Nchi yetu Jamhuri ya Afrika ya Kati iliathirika sana na hatuwezi kukubali tena watu warudi kuteseka. Ninaahidi kuwa karibu na wananchi wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, ili kutunza utulivu na amani katika nchi yetu , " ameongeza.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.