Pata taarifa kuu
ZANZIBAR-UCHAGUZI

Upinzani Zanzibar, walalamika viongozi na wafuasi wake kukamatwa

Mwenyekiti wa Chama cha ACT Wazalendo Maalimu Seif Sharifu Hamad amesema kuwa zaidi ya wanachama wake 280 wa chama hicho walikamatwa na Jeshi la Polisi hapo jana katika maandamano aliyo itisha kupinga matokeo ya Uchaguzi Mkuu Kisiwani humo.

Mgombea urais Zanzibar kupitia chama cha ACT Wazalendo Maalim Seif Sharif Hamad
Mgombea urais Zanzibar kupitia chama cha ACT Wazalendo Maalim Seif Sharif Hamad ACT WAZALENDO ZANZIBAR:twitter.com
Matangazo ya kibiashara

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Maalimu Seifu anashangazwa na kitendo cha Jeshi la Polisi kutumia nguvu kuwatawanya waandanaji wa chama hicho waliojitokeza kupinga matokeo.

Aidha katika hatua nyingine Maalimu Seifu amesema hadi hivi sasa hawajui alipo Naibu katibu Mkuu wa chama hicho Nasoro Mazurui.

Kwa upade wake Kamanda wa Jeshi la Polisi katika Mkoa wa Mjini Magharibi Awadhi Juma Haji ameiambia FRI Kiswahili kuwa jeshi hilo halimshikirIi kiongozi huyo na hana taarifa za Mahali alipo huku akisema sababu za kukamatwa kwa Wafuasi wa ACT Wazalendo ni kufanya maandamano yasiyo na kibali.

Katika hatua nyingine Kamanda Awadhi amesemakuwa hali ya ulinzi na usalama imeimarishwa Viswani humo nhuku viongozi wa Maalimu Seifu na wenzake wakitakiwa kuripotipi katika kituo cha jeshi hilo hadi pale watakapo kamilisha uchunguzi wao

Na ripota zetu wa Zanzibar, Martin Nyoni

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.