Pata taarifa kuu
ZANZIBAR-UCHAGUZI

Mwinyi atangazwa mshindi Zanzibar, Seif apinga matokeo

Hapo jana majira ya usiku Tume ya Uchaguzi Zanzibar imemtangaza Dr. Hussein Mwinyi kuwa msindi wa kiti cha Urais wa Serikali ya Mpinduzi Zanzibar, matokeo yaliyo tangazwa na Menyekiti wa ZEC Jaji Msataafu Hamid Mahmoud Hamid wakati kinara wa Upinzani Kisiwani humo akiwa anashilikiliwa na Jeshi la Polisi

Rais mteule wa Zanzibar, Hussein Mwinyi
Rais mteule wa Zanzibar, Hussein Mwinyi YouTube Screenshot
Matangazo ya kibiashara

Akizungumza mara baada ya kutangazwa Rais Mteule Dr. Hussein Mwinyi amesema swala la kuwaunganisha wa Zanzibar mara bada ya pilika za uchagzui kukamilika jambo muhimu pindi atakapo kabidhiwa ofisi.

 

Wakati tume ikikamilisha zoezi lakuweka adharani matokeo ya Uchaguzi Mkuu kinara wa upinzani na aliyekuwa mgombe Urais Maalimu Seifu Sharifu Hamad alikamatwa na Jeshi la Polisi kwa kile kilicho tajwa kuhamasiha maandamano.

 

Vikosi vya ulinzi na usalama vimetumia mabomu ya kutoa machozi kuwa tawanya dazani ya waandamanaji walionza kujitokeza kuitikia wito wa Maalimu Seifu kufanya maadamano

Dr. Hussen Ali Mwinyi anakuwa rais wa awamu ya nane ya serikali ya Mapinduzi Zanzibar akiingia madarakani kwa kukupata kura asilimia   76.2 na mpinzania wake wa karibu Maalimu Seifu akipata Asimilia 19. 8 ya kura zote  zilizo pingwa

01:37

Ripoti ya kutangazwa matokeo ya Uchaguzi Mkuu Hapo jana Zanzibar- Martin Nyoni

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.