Pata taarifa kuu
GUINEA-SIASA-USALAMA

Uchaguzi wa urais Guinea: Maafisa wawili wa Tume ya Uchaguzi wajiuzulu

Kufikia sasa mshindi katika duru ya kwanza ya uchaguzi wa urais uliyofanyika siku ya Jumapili nchini Guinea hajatangazwa rasmi. Siku ya Alhamisi jioni Tume ya Uchaguzi ilitangaza matokeo mapya ya awali, lakini bado kunakosekana takwimu kutoka maeneo matatu.

Kabla ya kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi, polisi wa Guinea wanaendelea kutoa ulinzi mkali katika mitaa ya Conakry. Oktoba 21, 2020.
Kabla ya kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi, polisi wa Guinea wanaendelea kutoa ulinzi mkali katika mitaa ya Conakry. Oktoba 21, 2020. AP Photo/Sadak Souici
Matangazo ya kibiashara

Wakati huo huo maafisa wawili wa Tume ya Uchaguzi wamejiondoa kwenye zoezi la kujumlisha matokeo ya uchaguzi.

Makamishna hao wanalaani kile wanachodai "makosa makubwa" katika utaratibu wa kuhesabu kura.

Tume ya Uchaguzi, CENI, inatarajia kukutana tena leo Ijumaa, lakini maafisa wawili wa hiyo wamejiondoa katika zoezi la kujumlisha matokeo ya uchaguzi wakati ambapo mvutano unaendelea kuongezeka katika mji mkuu wa Conakry.

Katika taarifa iliyotumwa kwa wvyombo vya habari, Diogo Baldé na Marie Hélène Sylla, maafisa wawili wa CENI, wanalaani "makosa makubwa yaliyoonekana katika utaratibu wa kujumlisha matokeo ya uchaguzi".

"Uangalizi wetu ili kuhakikisha uwazi, kutoegemea na ukweli wa matokeo" haujazingatiwa, wameandika. Akihojiwa kwa njia ya simu, Marie Hélène Sylla amebaini: hajahudhuria zoezi hilo tangu Alhamisi na sio "kujiuzulu", lakini "kujiondoa". amepinga "mchakato", utaratibu wa kujumlisha matokeo ya uchaguzi katika ngazi ya Tume ya Uchaguzi.

CENI tayari imetangaza takwimu za maeneo 35 kati ya 38 ya nchi hiyo. Matokeo ya jimbo la Mamou bado hayajapatikana, na nje ya nchi, hususan DRC na Gambia, kulingana na msemaji wa Tume ya Uchaguzi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.