Pata taarifa kuu
LIBYA)UN-USALAMA

Libya: Pande hasimu zatia saini mkataba wa kudumu wa kusitisha mapigano "

Umoja wa Mataifa umetangaza leo Ijumaa, Oktoba 23, kufikiwa mkataba kamili na wa kudumu wa kusitishwa kwa mapigano nchini Libya kati ya kambi ya Khalifa Haftar huko Benghazi na ile ya serikali ya umoja wa kitaifa iliyoko Tripoli.

Amhimmid Mohamed Alamam (kushoto) Akiwakilisha kambi ya Haftar, na Ahmed Ali Abushahma kutoka serikali ya umoja wa kitaifa. wakisalimiana kwa kupeana mkono Oktoba 23 huko Geneva.
Amhimmid Mohamed Alamam (kushoto) Akiwakilisha kambi ya Haftar, na Ahmed Ali Abushahma kutoka serikali ya umoja wa kitaifa. wakisalimiana kwa kupeana mkono Oktoba 23 huko Geneva. Violaine Martin / UNITED NATIONS / AFP
Matangazo ya kibiashara

Kambi hizo hasimi wametia saini mkataba huo baada ya mazungumzo ya siku tano huko Geneva.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres leo Ijumaa amekaribisha mkataba wa kusitisha mapigano uliyofikiwa nchini Uswisi siku hiyo hiyo kati ya pande zinazokinzana nchini Libya, akibaini kwamba ni "hatua ya kimsingi kuelekea amani na utulivu nchini Libya ”.

Tangu mkutano wa Berlin mwezi wa Januari 2020, kamati tatu zimejadiliana ili kuindia Libya kwenye mgogoro huo. Mazungumzo ya Geneva, yalihusu maswala ya usalama na ya kijeshi. Kwa upande wa Stéphanie Williams, mkuu wa tume ya Umoja aw Mataifa nchini Libya, MANUL, amesema "bado kuna mengi ya kufanywa katika wiki zijazo", na ikiwa njia ya kufikia mkataba huu wa kudumu wa "kusitisha vita" imekuwa "ndefu na ngumu", kinachosalia kufanywa pia bado ni kigumu, n akitachukuwa muda.

Stéphanie Williams alihutubia, wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari kabla ya kutiwa saini kwenye mkataba huo, alitoa wito kwa vikosi vya kigeni vinavyopigana nchini Libya kusitisha uingiliaji wao katika masuala ya Libya, huku akizitaka baadhi ya nchi kuondoa mamluki wao na kuheshimu vikwazo vya silaha vilivyochukuliwa dhidi ya Libya, azimio ambalo baadhi ya nchi zimekuwa zikikiuka kwa miaka kadhaa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.