Pata taarifa kuu
MALI-ECOWAS-SIASA-USALAMA

Nana Akufo-Addo: Nina matumaini kuhusu kipindi cha mpito nchini Mali

Rais wa Ghana Nana Akufo-Addo, rais wa sasa wa Jumuiya ya Mataifa ya Afrika Magharibi (ECOWAS), katika ziara yake nchini Mali Jumapili Otoba 11 amesema kuwa ana "matumaini mazuri" kwamba viongozi wa mpito nchini Mali wataheshimu ahadi zao.

Rais wa sasa wa ECOWAS "amewahimiza viongozi wa mpito kukamilisha ratiba ya mchakato wa uchaguzi" (picha ya kumbukumbu)
Rais wa sasa wa ECOWAS "amewahimiza viongozi wa mpito kukamilisha ratiba ya mchakato wa uchaguzi" (picha ya kumbukumbu) John MacDougall/Pool/AFP via Getty Images
Matangazo ya kibiashara

"Kwa sasa, vitendo vyote vinavyofanywa na viongozi wa mpito vinatupa matumaini mazuri kwamba wanatekeleza ahadi twalizojikubalisha mbele yetu", alisema rais wa Ghana wakati wa mkutano mfupi na waandishi wa habari baada ya ziara yake.

Akiandamana na rais wa zamani wa Nigeria Goodluck Jonathan, mpatanishi katika mgogoro huu, na rais wa Tume ya ECOWAS, Jean-Claude Kassi Brou, Nana Akufo-Addo alikutana na rais wa mpito Bah N'daw, Kanali wa jeshi aliyestaafu, na makamu wa rais wa mpito, kiongozi wa mapinduzi, Kanali Assimi Goïta. Alikutana pia na Waziri Mkuu wa Mpito Moctar Ouane, Waziri wa zamani wa Mambo ya nje na mwanadiplomasia aliyebobea.

Kwa upande wale viongozi wa jumuiya ya kikanda, ECOWAS, wanasema viongozi wa mpito wa Mali wanapaswa kuendelee kwenye njia hiyo nzuri, kwa kuunda haraka Baraza la Mpito la Kitaifa (CNT), chombo cha kutunga sheria. Lakini wamesema lazima mambo yawekwe wazi haraka ili raius atakaye chaguliwa kidemokrasia akabidhiwe madaraka baada ya miezi 18. Rais wa sasa wa ECOWAS "amewahimiza viongozi wa mpito kukamilisha ratiba ya mchakato wa uchaguzi ili kufikia katika uchaguzi wa urais na wa wabunge katika kipindi walichokuabaliana", kulingana na taarifa iliyosomwa wakati wa mkutano na waandishi wa habari.

Rais wa Ghana pia alikutana na Waziri Mkuu wa zamani Boubou Cissé, mmoja wa watu kumi na moja, raia na wanajeshi, ambao bado wanazuiliwa tangu mapinduzi na ambaye Kanali Goïta alitangaza kuachiliwa Jumatano wiki iliyopita. Kuachiliwa huku ilikuwa moja ya madai ya ECOWAS. Moja ya madai mengine ya ECOWAS ni kuvunjwa kwa Kamati ya Kitaifa ya Wokovu wa Wananchi (CNSP).

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.