Pata taarifa kuu
MALI-ECOWAS-SIASA-USALAMA

Mali: ECOWAS yaondoa vikwazo vilivyowekwa tangu mapinduzi ya Agosti 18

Huu ndio mwisho wa vikwazo vilivyowekewa Mali tangu mapinduzi ya Agosti 18 dhidi ya Rais Ibrahim Boubacar Keïta. Jumuiya ya kiuchumi ya nchi za Afrika Magharibi imetangaza kuondoa vikwazo hivyo.

Mji mkuu wa Mali, Bamako, Agosti 9, 2018 (Picha ya kumbukumbu)
Mji mkuu wa Mali, Bamako, Agosti 9, 2018 (Picha ya kumbukumbu) REUTERS/Luc Gnago
Matangazo ya kibiashara

Tangazo la wakuu wa nchi na serikali za Jumuiya ya Kiuchumi ya Mataifa ya Afrika Magharibi (ECOWAS) hukusu Mali lilitolewa mchana wa Jumanne hii, Oktoba 6. Tangazo hilo limesainiwa na rais wa Ghana Nana Akufo-Addo, rais wa sasa wa ECOWAS, ambaye amesema kwamba, "kwa kuzingatia maendeleo jinshi Mali inaendelea kupiga hatua kwa hatua kwa yale iliyotakiwa kufanya kwa kurejesha taasisi zinazokubaliwa kikatiba, wakuu wa nchi za jumuiya ya ECOWAS wanaamua kuondoa vikwazo kwa Mali ”.

Safari za ndege zinatarajiwa kuanza tena. Wasafiri watafanya safari zao kutoka Mali kwenda katika nchi za jumuiya ya ECOWAS. Shughuli za kifedha pia zimeanza, huu ndio mwisho wa vikwazo vya kiuchumi.

Waziri Mkuu mpya wa Mali, Moctar Ouane, amechangia sana katika kuondolewa kwa vikwazo hivi. Katika siku za hivi karibuni, alikuwa akiwasiliana na marais wa nchi wanachama wa ECOWAS na alishiriki katika kuchukuwa uamuzi nchini Mali, akiwezesha kuondoa vikwazo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.