Pata taarifa kuu
ETHIOPIA-MISRI-SUDANI-USHIRIKIANO

Bwawa la Grand Ethiopian Renaissance kuanza kuzalisha umeme katika kipindi cha miezi 11 ijayo

Bwawa kubwa la kuzalisha umeme nchini Ethiopia ambalo limeshuhudia mvutano baina ya nchi hiyo, Sudan na Misri, linatarijiwa kuanza kuzalisha umeme katika kipindi cha miezi kumi na moja ijayo kulingana na taarifa ya rais Sahle-Work Zewde.

Mapema mwezi Julai viongozi wakuu wa Misri, Sudan na Ethiopia walikubaliana kwamba Addis Ababa itachelewesha ujazaji wa bwawa lake lililoko kwenye mto wa Blue Nile hadi mataifa hayo matatu yatakapofikia makubaliano juu ya mgawo wa maji ya mto huo.
Mapema mwezi Julai viongozi wakuu wa Misri, Sudan na Ethiopia walikubaliana kwamba Addis Ababa itachelewesha ujazaji wa bwawa lake lililoko kwenye mto wa Blue Nile hadi mataifa hayo matatu yatakapofikia makubaliano juu ya mgawo wa maji ya mto huo. REUTERS/Tiksa Negeri
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, huenda bwawa hilo likawa tayari limejaa baada ya kipindi cha mwaka mmoja wa kulijaza maji na sasa linatarajiwa kuwa bwawa kubwa zaidi la uzalishaji umeme katika bara la Afrika.

Mapema mwezi Julai viongozi wakuu wa Misri, Sudan na Ethiopia walikubaliana kwamba Addis Ababa itachelewesha ujazaji wa bwawa lake lililoko kwenye mto wa Blue Nile hadi mataifa hayo matatu yatakapofikia makubaliano juu ya mgawo wa maji ya mto huo.

Wakati huo Misri na Ethiopia zote ziligusia uwezekano wa kuchukua hatua za kijeshi kulinda maslahi yake, na kuibua hofu ya kutokea kwa mgogoro wa wazi.

Ethiopia imekuwa ikipaza sauti kuhusu nia yake ya kujaza bwala hilo, ambalo inasema ni muhimu kwa mahitaji yake ya umeme na maendeleo. Inasema mradi huo wa bwawa la umeme wenye thamani ya dola bilioni nne, utakuwa na uwezo wa kuzalisha megawati 6,450 na utasidia kuwaondoa mamilioni ya watu kutoka kwenye dimbwi la umaskini.

Misri kwa upande mwingine, inautegemea mto Nile kwa asilimia 97 ya mahitaji yake ya maji safi. Inasema bwana hilo linaweza kupunguza ugavi wake wa maji na kuwa athari mbaya kwa wakaazi wake. Sudan pia inategemea mto Nile kwa ugavi wa maji na imetoa mchango muhimu katika kuzileta pande mbili pamoja.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.